Nafasi Ya Matangazo

October 11, 2012

Daktari wa Macho akimfanyia uchunguzi mgojwa wa macho Upendo Kisese kutoka Segerea wakati Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick akishuhudia kwenye viwanja vya Biafra leo wakati wa maadhimisho ya siku ya macho duniani, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Afya bora ya macho na maendeleo ya Taifa sambamba na kauli mbiu hii, ujumbe mahsusi kwa wadau wa Afya ni: Amua kuwekeza sasa katika huduma za macho uepushe gharama za ulemavu wa kuona”.

Msimamizi wa Kitengo Cha macho Manispaa ya Ilala Ramadhani Msuya, akimpima mgonjwa wa macho  Ustadh Abuu Yusuph wakati wa Maadhimishohayo ambapo huduma hizo zinatolewa bure kwa siku nzima.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik, akikata Utepe kuzindua maandamano ya wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered kwaajili ya maadhimisho ya Siku ya macho duniani yaliofanyoka leo jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi wa taasisi ya Brien Holden Vision Istitute wakishirikiana na Standard Chartered kuandamana kutoka Posta  hadi kwenye viwanja vya Biafra kwaajili ya maadhimisho ya siku ya macho ambayo hufanyika kila Alhamisi ya mwanzo ya mwezi wa 10.
Meneja wa Ushirikiano wa Benki ya Standar Chartered Beda Biswalo, akiwaelekeza Kaimu Mkurugenzi wa Benki hiyo (katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam njia watakazopita kuandamana kwaajili ya maadhimisho ya siku ya macho duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo takwimu za tatizo la ubovu wa macho zilitolewa.
Posted by MROKI On Thursday, October 11, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo