Nafasi Ya Matangazo

October 31, 2012

Na Father Kidevu Blog
WAKATI zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya Redd’s Miss Tanzania 2012 kupatikana, mambo ndani ya kambi ya warembo 30 wanaowania taji hilo imekuwa ya hofu tupu, huku kila mshiriki akibaki kujiuliza nani atatwaa taji hilo. 

 Miss Redd’s Tanzania 2012 atajiwalia gari pamoja na fedha taslimu Sh milioni 8, katika kinyang’anyiro kinachotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl uliopo jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam siku ya Jumamosi. 

 Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika kambi yao hiyo iliyopo hoteli ya Giraffe, Mbezi Beach, Dar es Salaam warembo mbalimbali walisema washiriki wote kwa sasa wana hofu tupu. “Pamoja na kuingia 15 bora ya Redd’s Miss Tanzania mpaka sasa, lakini bado sina uhakika kama nitatwaa taji, maana kila mrembo namuona yuko bomba,” alisema Redd’s Miss Photogenic, Lucy Stephano. 

 Mpaka sasa washiriki wanne  waliofanikiwa kuingia hatua ya 15 bora ni Lucy pamoja na Mary Chizi aliyetwaa taji la Miss Sports Lady , Babylove Kalala aliyefanikiwa kushinda lile la Redd’s Miss Talent na Miss Top Model Magdalena Roy .

 Warembo hao wawili pia walizungumzia ugumu wa shindano hilo, huku Mary akisema kuna kazi kubwa na Babylove akidai kila kitu kwa sasa amekiacha mikononi mwa Mungu. Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga, ambao ndio waandaaji wa shindano hilo alisema, kila kitu kwa sasa kimekamilika na wana imani kubwa shindano litakuwa kali na la kuvutia. 

 “Tumekamilisha kila kitu, naamini atapatikana mrembo mkali zaidi ambaye atatuwakilisha vema katika mashindano ya dunia,” alisema. Naye Meneja wa kinywaji cha Redd’s Original walio wadhamini wakuu wa shindano hilo, Victoria Kimaro, alisema huu ni wakati sahihi wa kumpata mshindi bomba mwenye vigezo.

 “Kwa jinsi mambo yalivyo, nawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi siku ya shindano, maana hili litakuwa ni shindano la kipekee,” alisema. Shindano hili la Redds Miss Tanzania 2012 linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji cha Redds Original.
Posted by MROKI On Wednesday, October 31, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo