Meneja Airtel Money John Ndunguru na Mkuu wa huduma za kibenki Mwanahiba Mzee kwa pamoja wakikabidhiana mikataba mara baada ya makubaliano ya ushirikiano wa Airtel na Bank of Afrika katika kutoa huduma ya Airtel money kupitia matawi ya bank hiyo yote yaliyopo Tanzania. Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika Makao makuu ya Airtel Morocco Jijini Dar es Salaam. wakishuhudia Katikati ni Mmoja ya wakala mkubwa wa Airtel money kutoka kampuni ya Connexions bwn Shyamkumar Balakrishnan (katika) na kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando (kushoto) akiongea wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wa kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel na Bank of Afrika katika kutoa huduma ya Airtel money kupitia matawi ya bank hiyo yote yaliyopo Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika Makao makuu ya Airtel Morocco Jijini Dar es Salaam. pichani kulia ni mkuu wa kitengo cha IT Bank of Afrika bwn. Willington Munyanga , akifatiwa na Mkuu wa huduma za kibenki Mwanahiba Mzee na anayefatia ni Meneja Airtel Money John Ndunguru.
Meneja Airtel Money John Ndunguru na Mkuu wa huduma za kibenki Mwanahiba Mzee wakipitia mkataba mara baada ya makubaliano ya ushirikiano wa Airtel na Bank of Afrika katika kutoa huduma ya Airtel money kupitia matawi ya bank hiyo yote yaliyopo Tanzania.
*****
Huduma bora na ubunifu wa huduma mpya zinazokidhi matarajio ya wateja ni moja ya silaha muhimu katika kukuza wateja waliopo pamoja nakuongeza idadi ya wateja wapya, Kutokana na msingi huu BANK OF AFRICA TANZANIA ina furaha kuanzisha ushirikiano na AIRTEL TANZANIA katika kutoa huduma ya Airtel money kupitia matawi yake yote yaliyopo Tanzania.
Ushirikiano huu wa kibiashara unatoa fursa kwa wasambazaji wa huduma za Airtel Money kupata PESA za mtandao pasipo usumbufu wowote. Katika tukio la leo baina ya BANK OF AFRICA na AIRTEL TANZANIA tunapenda pia kutangaza uanzishwaji wa mikopo kwa wasambazaji wa Airtel money ili kukuza mitaji itakayowawezesha kulikabili soko shindani la biashara hii.
Makubaliano haya yanayotiwa saini leo yanaendelea kuboresha huduma za kifedha zitolewazo kupitia mitandao ya simu za mkononi kupitia BANK OF AFRICATANZANIA. Ushirikiano huu wa Huduma ya Airtel money unawalenga mawakala wakubwa na wa kati pamoja na wasambazaji wadogo wa Airtel Money katika kupata pesa za mtandao zitakazowawezesha kuendesha biashara zao kwa ufanisi zaidi, sambamba na hilo pia Mawakala na wasambazaji wa Airtel Money watapatiwa mikopo itakayowawezesha kukuza biashara zao, mikopo hiyo itakuwa kati ya shilingi Millioni 10 hadi 100.
Kwa upande wake Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Airtel Money Godfrey Mugambi amesisitiza kwamba ushirikiano wa Airtel Tanzania na BANK OF AFRICA TANZANIA ni moja ya mkakati wa kampuni yake katika kuendelea kuboresha na kufikisha huduma za kifedha nchini kote.
Hii ni njia rahisi sasa itakayowawezesha wasambazaji wetu wa Airtel Money wakubwa kuwafikia mawakala wengi na kuokoa muda na gharama walizokuwa wanazipata kutafuta pesa za mtandao.
Airtel inatambua ongezeko la mahitaji ya huduma za kifedha zenye usalama, uhakika, katika soko la Tanzania na ni kwa sababu hizi Kampuni ya Airtel imeingia makubaliano na BANK OF AFRICA TANZANIA kutoa huduma ya Airtel Money nakurahisha zaidi upatikanaji wa huduma hii kwa wateja.
Huduma za Airtel Money zitawawezesha makundi yote nchini yaani yale yaliyofikiwa na taasisi za kifedha kama mabenki na yasiyo fikiwa na mabenki kupata huduma za kifedha kwa urahisi Kupitia mtandao wa simu ya mkononi.
Aidha Huduma ya Airtel Money inatoa fursa kwa taasisi, mashirika mbalimbali, kujenga uwezo wa matumizi makubwa ya teknologia ikiwa ni pamoja na kurahisisha huduma za mfumo wa malipo kwa ajili ya bidhaa au huduma mbalimbali.
Huduma za Airtel Money zinapatikana nchi nzima kwa wateja wote wa malipo ya kabla na ya baadaye, Airtel money ina mawakala zaidi ya elfu 20,000 nchi nzima wakitoa huduma mbalimbali ikiwemo kuwaunganisha Wateja na huduma ya Airtel Money bure bila ya malipo ya uandikishwaji.
0 comments:
Post a Comment