Watoto wakazi wa Ubungo External jijini Dar es Salaam wakichota maji na kuoga katika mabomba yaliyokatwa na kumwaga maji hovyo katika kipande cha barabara kinacho unganisha barabnara ya Mandela na Ubungo Maziwa ambacho hivi sasa kunajengwa kwa kiwango cha lami.
Kumwagika hovyo kwa maji hayo ni uharibifu tosha wa rasilimali hiyo ambayo inahitajiwa na wakzi wengi wa jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake hivyo Mamlaka husika ya usimamizi na usambazaji wa maji safi jijini Dar es Saalaam DAWASCO hawana budi kuyafunga mabomba haya kwa muda kupisha ukarabati huo wa barabara ili kuzuia uharibufu huo wa maji bila sababu. Maji haya endapo yangefungwa yasimwagike huenda yangewafikia wakazi wa jiji ambao hupata maji kidogo.
Kijiko kikiendelea nakazi ya kuchimba barabara hiyo na kukata mabomba ya maji yaliyopo kando kando ya barabara hiyo.
0 comments:
Post a Comment