Nafasi Ya Matangazo

September 11, 2012

Na Father Kidevu Blog, Pangani
MBUNGE wa Viti maalum Amina Mwidau (CUF), amekabidhi mashine ya kusumia maji yenye dhamani ya Shilingi milioni 5 kwa wanachi wa Kijiji cha Mwera Wilayani Pangani ikiwa ni sehemu ya ahadi yake kwa wakazi hao.

Akikabidhi mashine hiyo Mwidau, aliwataka wananchi kukiunga mono chama cha CUF, ili kuweza kujenga demokrasia na ukombozi wa kweli kwa Taifa.

Mbunge  huyo amewataka wananchi kuhakikisha wanawakataa katika masanduku ya kura itakapofika mwaka 2015 ili Bunge hilo liwe na wabunge wengi kutoka vyama vya upinzani.

“Leo nchi imekuwa na matatizo kila kona kutokana na kusekana na wabunge wa kweli ambao wana uchungu wa kuwatetea wananchi na ninayasema haya mchana kweupe  idadi ya wabunge wengi wa CCM imekuwa ni kikwazo kwetu sisi wapinzani.

“Hata nanyi wananchi wa Mwera inalitambua hilo, na kutokana na hali hii na hata mbunge mwenzangu wa jimbo hilo ambaye anatokana na CCM hana muda wa kurudi tena tangu mlipomchangua. Kwa zaidi ya miaka miwili sasa hajarudi tena n hata leo hii mna tatizo la maji kwa mota kuungua hana habari nanyi.

“Ili kuweza kupambana na mfumo huu mbobu ulioandaliwa na CCM kutokana na sera zake kuwa mbovu tunahiaji kujenga nchi kwa kuwa na viongozi majasiri kama Profesa Lipumba ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipigania haki za Watanzania.

“Ninakabidhi mashine hii yenye dhamani zaidi ya Sh milioni 5 ili kuweza kutatua kero ya maji katika kijiji hiki cha Mwera, ninajua uchungu wa maji kwani hali hii iliyopo sasa wanaopata taabu ni wanawake wenzangu na watoto ambao hutumia muda mwingi kutafuta maji badala ya kufanya shughuliza uzalishaji maji,” alisema Mwidau
Posted by MROKI On Tuesday, September 11, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo