Wasanii kutoka kundi la sanaa la baba watoto lenye maskani yake Mburahati jijini Dar es salaam, wakicheza ngoma ya Kibati wakati wa tamsha maalum la kuhamasisha wananchi kushiriki katika utoaji maoni yao katika Katiba Mpya. Tamasha hilo lilifanyika katika viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam leo na kuratibiwa na Kikundi cha Sheria Sheria na Haki za Binadamu Cha TIFPA (Chama Cha Wanafunzi aliofadhiliwa na Shirika la Ford Foundation la Marekani)
Mmoja wa wasanii wa kundi hilo akiimbisha nyimbo hiyo ya kibati wakati wa tamasha hilo leo.
Meya wa Manipaa ya Temeke, Mstahiki Meya Maabad Hoja ndiye alikuwa mgeni rasmi na kufungua tamasha hilo la Kuhamasisha Umma juu ya Katiba Mpya. wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi na kutoa maoni yao juu ya katiba mpya.
Mwenyekiti wa Kikundi Cha Sheria na Haki za Binadamu Cha TIFPA (Chama Cha Wanafunzi waliofadhiliwa na Shirika la Ford Foundation la Marekani) akizungumza wakati wa Tamasha hilo na kutolea ufafanuzi maswali ya wananchi juu ya masuala mbalimbali ya Katiba Mpya na kazi za TIFPA.
Wananchi walihamasishwa kujitokeza katika Utoaji maoni juu ya Katiba Mpya na kundi la BABA WATOTO am,bao walionesha ufundi wao katika Sarakasi.
Maigizo yalifanyika ili kuonesha ni jinsi gani wasipo shiriki katika Zoezi la Utoaji Maoni ya Katiba mpya litakavyo waathiri hapo baadae kwa yale wanayopenda yawepo katika katiba maana hayata kuwepo.
Ilifika zamu sasa ya igizo la utoaji maoni juu Katiba Mpya na hapa wananchi wakiwa katika mkutano huo wakitoa maoni yao
Wanawake nao wanapaswa kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo la Katiba Mpya na hapa kundi la Baba watoto liliwahamasisha vyema akina mama wakazi wa Mbagala kujitokeza kwa wingi siku hiyo ikifika.
Mvutano ulitokea baada ya wananchi hao kushindwa kutoa maoni baada ya Mzee mmoja kukalipia Mkewe na kumtaka aondoke katika utoaji wa maoni ya katiba mpya.
wananchi walitoa maoni yao juu ya walicho jifunza katika maigizo na nyimbo za Kundi la Baba watoto...
Wanafunzi nao wanahaki ya kutoa maoni yao juu ya Katiba Mpya...kama huyu wa Shule ya Vikindu kidato cha kwanza akieleza mafunzo aliyo yapata katika maigizo hayo na kuwataka wananchi wenzake wabadilike.
Mwitikio wa watu ulikuwa mzuri sana
Vitabu hivi viligawiwa kwa wananchi wengi walio kuwa na shauku ya kutaka kujifunza yale yaliyopo katika Katiba ya Sasa ili katika Marekebisho ya Katiba Mpya wajue cha kuzungumza.
Maoni mbalimbali yalitolewa na wakazi wa Mbagala juu ya umuhimu wao kushiriki katika Katiba mpya.
Vitabu viligawiwa sasa kwa wananchi na walivigombea kama njugu. Kesho kutafanyika mkutano kama huo maeneo ya Buguruni jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea mikoa ya Mwanza, Arusha, na Mbeya katika awamu ya kwamnza.
0 comments:
Post a Comment