Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Raymond Mbilinyi (kulia) akikata utepe kuzindua kitabu chenye Ripoti ya Uwekezaji ya Kimataifa 2012 sambamba na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou.
Pichani Juu na Chini ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Dunia ya Uwekezaji 2012 yenye kauli mbiu 'Sera Kuelekea Kizazi Kipya katika Uwekezaji' ambapo amewasisitiza watunga sera wa Tanzania kutumia rasimu ya Sera ya Uwekezaji ya Maendeleo Endelevu kwa mwaka 2012 kama kipaumbele katika kuunda sera za Kitaifa za Uwekezaji. Kushoto ni Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(UNIC) Bi. Stella Vuzo.
Baadhi ya Maafisa wa Umoja wa Mataifa nchini waliohudhuria uzinduzi wa World Investment Report 2012.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Raymond Mbilinyi akiwasilisha Ripoti hiyo ya Mwaka 2012 ambapo amezungumzia zaidi mazingira ya uwekezaji Tanzania huku akigusia mwelekeo, changamoto na fursa zinazopatikana.
Bw. Raymond Mbilinyi ameweka wazi kuwa mujibu wa Ripoti hiyo Tanzania kwa sasa imepiga hatua katika kuboresha miundo mbinu haswa ya Barabara miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki.
Dkt. Alberic Kacou (kushoto) na wadau wakifuatilia uwasilishwaji wa Ripoti ya Fursa za Uwekezaji 2012.
Pichani ni Minongoni mwa Mabalozi, wawakilishi wa Serikali, wakuu wa mashirika ya Maendeleo, wawakilishi wa mashirika ya kijamii katika uzinduzi huo.
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo akimkaribisha Dkt. Kacou na Bw. Mbilinyi (hawapo pichani) kuzindua rasmi 'World Investment Report 2012'.
Sasa imezinduliwa rasmi.
Mkurugenzi wa Zamani wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bw. Emmanuel Ole Naiko akitoa maoni yake kuhusiana na Ripoti ya Kimataifa ya Uwekezaji 2012.
Pichani Juu na Chini Wadau wa Sekta ya Uwekezaji, Maafisa wa Umoja wa Mataifa, Mabalozi pamoja Wawakilishi wa Idara mbalimbali za Serikali waliohudhuria Uzinduzi huo.
Dkt. Alberic Kacou na Mkurugenzi wa Zamani wa kituo cha Taifa cha Uwekezaji chini Bw. Emmanuel Ole Naiko wakipeana mkono wa Pongezi baada ya kuzindua Ripoti ya Kimataifa ya Uwekezaji 2012.
Dkt. Kacou akibadilishana mawazo na wageni waalikwa baada ya uzinduzi huo.
Bw. Emmanuel Ole Naiko (kulia) na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UNDP) Bi. Louise Chamberlain wakijadili kuhusu umuhimu wa matumizi ya Ripoti za Uwekezaji katika kukuza uchumi wa nchi.
0 comments:
Post a Comment