Nafasi Ya Matangazo

June 13, 2012

Mshambuliaji wa timu ya Mbeya chini ya umri chini wa miaka 17 wa Mbeya Seleman Victor (kushoto) akimpiga chenga mlinzi wa Arusha Mathew Jackson wakati wa mechi ya ufunguzi wa michuano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa katika uwanja wa Kumbu Kumbu ya Karume jijini Dar es Salaam Jumatatu (Juni 11, 2012). Mbeya walishinda 2-1.

Timu ya soka ya wanawake wenye umri chini ya miaka 17, imeifunga wenzao wa Lindi  4-0 kwenye muendelezo wa michuano ya Airtel Rising Stars uliochezwa jana asubuhi, Jumanne Juni 12. Magoli ya Temeke yaliwekwa kimiani na mshambuliaji hatari wa timu hiyo Fatuma Iddi kwenye dakika ya 13 na 19. Arafa Abdul waliwafungia Temeke goli la tatu huku Niewel Halafan akimalizia kazi kwenye dakika ya 58.

Wakati huo huo, timu ya Mpira wa Miguu ya Mbeya iliifunga timu ya Arusha mabao 2-1 katika pazia la kufungua mchezo wa fainali Ngazi ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa 17 yanayojulikana kama Airtel Raising Stars uliofanyika Jumatatu, Juni 11 ya wiki hii kwenye Uwanja wa Karume ,Dar es Salaam.Huku michuano hiyo ikiwa imetanguliwa na mechi ya wasichana baina ya Mikoa hiyo miwili huku Mbeya wakisinda 3-2.

Timu ya Arusha ya wavulana walifungua mechi hiyo kwa kasi lakini nguvu zao hazikuweza kuzaa matunda kabla ya vijana wa Mbeya kufunga goli dakika ya tisa kupitia mchezaji wake Mussa Msape.Goli hilo  la timu ya Arusha liliwafanya wachezaji hao kufikiria kutimiza   ndoto zao kuwa za kweli ambapo  dakika ya 24  mchezaji Shabaaan Jabir wa Arusha aliwatoka walinda mlango wa Mbeya na kupachika goli hilo.

Ndoto zao zilizimwa kwa goli la ushindi la timu ya Mbeya liliweka kinywani na mshambuliaji Stanley Kaduma aliyokuwa ni pasi nzuri kutoka kwa washambuliaji wa mbele. Huku kipindi cha pili kikiwa kimetawaliwa na pasi na kukosa magoli. Mbeya wasichana walipata goli lao kwa kwanza dakika ya saba kupitia mchezaji wake Lucia Venance huku dakika ya 25 Vaileth Mcholuosi akipachika goli la pili huko la mwisho likiwekwa kinywani na Naomi Lucas dakika ya 40 huku timu ya Arusha magoli yale yalifungwa dakika ya 12 kupitia Irine Venance na Venance huyo huyo kupachika goli la pili dakika ya 27.

Akizungumza wakati wa kufungua nusu fainali za  mashindano hayo ya wiki moja ,Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema kuwa Airtel Tanzania wamejikita katika kusaidia na kukuza mchezo wa mpira wa miguu na kuishukuru serikali pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa ushirikiano wake.

Kwa upande wa Rais wa TFF, Leodegar Tenga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kufungua michuano hiyo aliwataka Makampuni ya simu za mkononi kuwekeza katika program ya  soka la Vijana. Airtel Raising Stars kwa mwaka huu iliwashinrikisha shule za sekondari kutoka Mikoa ya Dar e sSalaam,Arusha, Mbeya na Lindi.  Washindi watatu kutoka kila timu kwenye michuano hiyo watachaguliwa kujiunga na Klinicki ya kimataifa ya mpira wa miguu itakayofanyika Nairobi August mwaka huu.
Posted by MROKI On Wednesday, June 13, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo