Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk amesema licha ya fujo ambazo zilitokea May 26 na 27 Usalama umeimarishwa vya kutosha na kuwataka Watalii waendelee kuja kufanya shuguli zao bila ya woga wowote.
Amesema Serikali inabeba jukumu la usalama wa Wageni ambao wanakuja Zanzibar na kufahamisha kuwa fujo lililotokea halikuathiri Sekta ya Utalii na maeneo yake muhimu.
Waziri Mbarouk ameyaeleza hayo alipokuwa akizungumza na Wawakilishi wa Mabalozi waliopo Nchini kuhusiana na fujo lililotokea jana na juzi kufuatia kukamatwa kwa kiongozi mmoja wa Jumuiya ya Kidini ya UAMSHO.
Amefahamisha kuwa maeneo muhimu ya Utalii yakiwemo Mji Mkongwe,Fukwe za bahari na Hoteli ni sehemu salama ambazo watu wanajishughulisha na kazi zao za kawaida na kuwaomba Mabalozi hao kuwafahamisha vyema wenzao kile ambacho kimetokea.
Amesema Jumatatu ya leo Afisi za Serikali na zile za binafsi ziliweza kufanya kazi ambapo kwa upande wa wananchi wa kawaida nao waliweza kuendeleza harakati zao za kila siku kutokana na hali kuwa salama.
Mbarouk ameeleza kuwa Jeshi la Polisi kwa ufanisi mkubwa liliweza kutuliza vyema fujo za waandamanaji bila ya kuwepo taarifa yoyote ya kifo au kujeruhiwa kwa mtu yeyote.
Waziri Mbaruk amesema kilichotokea ni watu kutumuia uhuru wao wa kidemokrasia wa kuelezea hisia zao ambazo baadae ziliashiria vitendo vya vurugu jambo ambalo liliwasababisha Polisi kuchukua hatua za kutuliza vurugu hizo.
Mbarouk amesema Serikali imejipanga vyema kuhakikisha inaendelea kuilinda haki ya kidemokrasia bila ya kutokea vitendo vyoyote vinavyoashiria kuhatarisha amani Nchini.
Amesema Taarifa ya Serikali imetolewa Jana na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud ambayo iliagiza vikosi vyote vya ulinzi kuwa macho kwa lengo la kutuliza usalama sambamba na kuwakamata wale wote waliohusika na fujo hizo.
Kwa upande wao Wawakilishi wa Mabalozi hao walimweleza Waziri huyo kuhakikisha amani inarudi kama kawaida ili watu waweze kuishi bila ya hofu Mkutano huo
0 comments:
Post a Comment