Pichani
kati ni Bw. Richard Muyungi ambaye ni Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya
mazingira ofisi ya makamu wa rais baada tuu ya kupewa uwenyekiti wa
kamati ya dunia ya sayansi mabadiliko ya tabia nchi, huko Durban africa
ya kusini na kuanza kazi rasmi katika mutano unaoendelea hapa ujerumani.
(Evelyn Mkokoi)
|
Mkurugenzi
msaidizi wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais bw.
Richad Muyungi akiwa katika Ofisi yake mjini Bonn Ujerumani
akiiwakilisha Tanzania kama mwenyekiti wa kamati ya dunia ya Sayansi na
taaluma ya mabadiliko ya tabia nchi, kazi hiyo ameianza rasmi katika
mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi unaoendela hapa Bonn
Ujerumani.
Tanzania
kwa mara ya kwanza imepata nafasi kwa miaka miwili ijayo ya kuongoza
Kamati ya umoja wa mataifa ya sayansi na taaluma ya mabadiliko ya
tabia nchi, chini ya mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya
tabia Nchi. Kamati imeanza kazi rasmi jana wiki hii, wakati wa ufunguzi
wa Mkutano wa 36 wa mabadiliko ya tabia nchi. Hayo yameelezwa leo
katika mahujiano maalum na ofisa Mkuu wa programu ya Uendeshaji ya
Sekretarieti ya Mkataba huu Bi Hanna Hoffmann, hapa Bonn, Ujerumani.
Bi
Hanna Ameeleza kuwa Bw. Richard Muyungi ambae ni Mkurugenzi Msaidizi wa
Idara ya mazingira kutoka katika ofisi ya Makamu wa Rais amepewa
dhamana hiyo na nchi zote duniani wanachama wa mkataba huu kutokana na
uzoefu wake mkubwa katika diplomasia ya mabadiliko ya tabianchi na
upeo wa kutosha juu ya taaluma nzima ya sayansi ya mabadiliko ya
tabianchi. “Bw. Muyungi ni mwana diplomasia aliyebobea katika masuala
ya mabadiliko ya tabianchi, ana elimu ya kutosha katika eneo hili na ni
mzoefu sana na amekuwa akihudhuria na kuongoza mkutano mingi ya
mabadiliko ya tabianchi hasa zaidi akiongoza kundi la nchi
zinazoendelea, hivyo naamini kabisa, uteuzi wake ni muafaka na ataongoza
vizuri kamati hii na masuala yote muhimu kama ulivyoona mwenyewe
alivyoongoza leo mkutano kuhusu kilimo na mabadiliko ya tabianchi .” Alisisitiza.
Bi
Hanna aliongeza kuwa Kundi la nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania ina
nafasi kubwa zaidi ya kujifunza na kutumia njia za kuhimili na
kukabilina na mabadiliko ya tabia nchi zaidi kutokana na nafasi yake ya
uwenyekiti wa Kamati hii.
Kwa
Upande wake Bw. Richard Muyungi ameeleza kuwa uteuzi huu uliofanyika
rasmi Desemba mwaka jana na nchi zote wanachama huko Durban Afrika ya
kusini, na kuanza rasmi leo, ni heshima kwa nchi na nafasi ya pekee
kwa Tanzania kuweza kujifunza mengi na kupata fursa mbali mbali za
kuweza kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi
zinazoikabili Tanzania ikiwemo uhaba wa mvua, mafuriko, kuongezeka kwa
kina cha bahari na, mvua zisizotarajiwa, nabaadhi ya maeneo ya nchi kuelekea kuwa janga kutokana na mabadiliko haya
Mkutano
huu unaoendelea hapa mjini Bonn Ujerumani, ni sehemu ya maandalizi ya
Mkutano wa Dunia wa mabadiliko ya tabia nchi, ambao utawakutanisha wakuu
wa nchi duniani utakaofanyika mjini Doha,Qatar, Novemba mwaka huu.
Aidha utatoa mchango katika mkutano wa wakuu wa nchi kuhusu Maendeleo
endelevu (Rio+20) utakaofanyika huko Rio, nchini Brazil baadaye mwezi
Juni.
Pamoja
na masuala ya Kilimo na mabadiliko ya tabianchi, Kamati hii pia
inatafuta muafaka kuhusu suala la matumizi ya sekta ya misitu katika
kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuzingatia maslahi ya nchi
zenye misitu inayonyonya gesi hizi, na taratibu za kusimamia na
kutekeleza miradi ya kupunguza hewa ukaa katika nchi zinazoendelea bila
kuathiri maendeleo ya nchi hizi. Aidha katika mkutano huu, Masuala ya
upatikanaji wa fedha ili kukabiliana na mabadilkio ya tabianchi kwa nchi
maskini duniani na suala la nchi zilizoendelea kuongeza juhudi za
kupunguza gesijoto zinazosababisha mabadiliko ya tabianchi yamepewa
kipaumbele.
0 comments:
Post a Comment