MSHAMBULIAJI wa Simba SC, Emmanuel Arnold Okwi anaweza akauzwa kwa klabu moja ya Austria kwa dau la dola za Kimarekani 500,000 (zaidi ya Sh. Milioni 750 za Tanzania) na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyewahi kuuzwa kwa ‘bei chafu’ zaidi Simba SC.
Kwa sasa, Mbwana Ally Samatta aliyeuzwa kwa dau la dola za Kimarekani 100,000 kwenda Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) msimu uliopita, ndiye anashikilia rekodi ya mchezaji wa Simba kuuzwa bei ghali zaidi.
Habari za ndani kutoka Simba, ambazo BIN ZUBEIRY imezipata Zinasema kwamba, Okwi mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, mwenye umri wa miaka 19 aliyetua Simba mwaka 2010 akitokea SC Villa ya Uganda anatakiwa na klabu hiyo kwa dau hilo tamu.
Ofa hiyo tayari iko mezani kwa Simba na kwa sasa inafanyiwa kazi kabla ya wakati wowote kutangazwa rasmi kuuzwa kwa mchezaji huyo, aliyesajiliwa na Wekundu wa Msimbazi, kwa dau la dola za Kimarekani 5000.
0 comments:
Post a Comment