Nafasi Ya Matangazo

May 03, 2012

 Mkazi wa Kinyenze akisukuma baiskeli yake akipita barabara ya Kinyenze
 Barabara ikionesha majani
Wananchi wa Kitongoji cha Kinyenze katika Kijiji cha Kipera, Kata na Tarafa ya Mlali Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro wameimba Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kuwachongea barabara yao kati ya Kipera na Kinyenze.

Wakizungumza kwa nyakati Tofauti Kijijini hapo wakazi hao wamesema barabara hiyo ina miaka mingi sana haijawahi kuchongwa na Greda kuisafisha.

“Barabara hii imekuwa ni kero kubwa sana kwetu hasa kipindi cha mvua ambapo mashimo na madimwi ya maji huwa mengi sana”, alisema Bakari Kimbwego.

Nae mkazi mwingine wa Kijijini hapo Omari Sisira amesema kuwa Wilaya ya Mvomero inapaswa kuwachongea bara bara hiyo ili nao wanufaike kama maeneo mengine yanavyopata huduma safi za usafiri.

Wananchi hao wamemuomba Diwani wa Kata yao ya Mlali, Juma Mrangi pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo, Amos Makala kuwasaidia barabara hiyo ichongwe.

Barabara ya Kinyenze hadi Kipera inayokadiriwa kuwa na uremfu wa Kilometa 2.5 ilikuwa ni barabara ya zamani ya Iringa na tangu ihamishwe enzi za mkoloni barabara hiyo iliyokuwa na kiwango cha lami haijafanyiwa matengenezo.
Posted by MROKI On Thursday, May 03, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo