Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) Paul Chizi (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi safari za ndege hiyo kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza wikendi hii.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) Paul Chizi akiongea na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza mara bada ya kuzindua safari za ndege mpya ya Shirika hilo aina ya Boeing 733-500 wikendi hii.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) Paul Chizi akiwa kwenyedaraja la ‘Business Class’ kwenye ndege mpya ya ATCL aina ya Boeing 737-500 wakati wa uzinduzi wa Safari za ndege hiyo
Mhudumu wa Ndege wa ATCL ambaye hakufahamika jina mara moja akimhudumia mmoja wa abiria wakati wa uzinduzi wa safari za ndege ya ATCL aina ya Boeing 737-500.
Ndege ya ATCL aina ya Boeing 737-500 inavyoonekana kwa mbele
Wahudumu wa ndege wa Shirika la ATCL wakipozi mbele ya Kamera ya blogu hii.
Abiria wakishuka kwenye ndege aina ya Boeing 737-500 ya ATCL kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati wa uzinduzi wa safari za ndege hiyo wikendi hii. Ndege hiyo itafanya safari za kila siku za Dar es Salaam-Kilimanjaro-Mwanza mara mbili kwa siku.
Na Mwandishi wetu.
MARA baada ya wiki moja tu baada ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kupata ndege aina ya Boeing 737-500 iliyoanza rasmi safari za Dar es Salaam-Kilimaanjaro-Mwanza wikendi hii, Shirika hilo limeanza mchakato utakayoliwezesha kupata ndege nyingine kati ya wiki tatu au sita zijazo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya safari hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Paul Chizi alisema shirika lake linatarajia kupata ndege nyingine aina ya Boeing ambayo italiwezesha shirika hilo kufanya safari za nje zikiwemo Dar es Salaam-Lusaka, Dar es Salaam-Harare and badae Dar es Salaam-Dubai.
“Tumeanza utekelezaji wa mpango kazi wetu wa muda mrefu ambao utatuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
“Katika mpango wetu ,tunatarajia kupata ndege nyingi na bora zaidi. Kwakuanzia,tunarajia kupata ndege nyingine katika kipindi cha wiki tatu mpaka sita na ndege hiyo itatuwezesha kuanza safari za kimataifa,’ alisema Chizi.
Chizi aliwataka wananchi pamoja na mashirika mbalimbali kuunga mkono jitihada za Shirika lake na kuahidi kuwa shirika hilo litazingatia utoaji wa huduma bora kwa bei nafuu. “Mafanikio ya shirika yatategemea mchango wa wadau mbali mbali. Tunaomba wananchi watuunge mkono ilituweze kupata mafanikio zaidi,” alisema.
Chizi alisema kuwa katika wiki chache zilizopita kampuni yake ilizindua tovuti ambayo itasaidia katika kuboresha huduma ya ukataji tiketi kwa wateja kwa wakati wao na kuboresha utoaji huduma wa kampuni.
“Kitu cha kujivunia ni kuwa wateja sasa wanaweza kutaka tiketi kupitia mtandao bila kufika katika ofisI zetu au kupitia mawakala wetu kama ilivyo zamani,” alisema.
Nae Jaji Mstafu wa Mahakama Kuu ambaye alipata nafasi ya kusafiri kwa kutumia ndege mpya ya shirika hilo aliomba Serikali kutoa ruzuku kwa Shirika hilo na kusisitiza kuwa uboreshaji wa shirika hilio utaongeza pato la taifa kupitia sekta ya Utalii.
0 comments:
Post a Comment