Nafasi Ya Matangazo

April 20, 2012

Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja (kulia) amekutana naMwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Bw. Alberic Kacou ofisini kwakejijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kuelekea Dodoma ambapo vikao vya Bungevinaendelea.

Mh. Ngeleja amekutana na Mwakilishi huyo baada ya kuwasilikutoka katika mkutano wa kimataifa ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa unaohusuNishati uliofanyika nchini Ubelgiji. 

Mh. Ngeleja aliiwakilisha Tanzania katika sekta ya Nishatiambapo Umoja wa Mataifa unategemea Nishati kuwafikia watu wote ifikapo Mwaka2030.

Mh. Ngeleja amesema kuwa pamoja na changamoto zilizopo haswaupatikanaji wa fedha, Serikali ya Tanzania imedhamiria kusambaza nishati nchiniTanzania (yenye watu zaidi ya milioni 45) kutoka asilimia 18.5 hadi asilimia 30ifikapo mwaka 2015.

Naye Mwakilishi wa Umoja wa Matifa amemshukuru Waziri kwajitihada zake kupitia wizara hiyo na akasisitiza kuwa Nishati kwa kila mtu nihaki ya msingi hivyo uharakishwaji wa mpango huo wa nishati kwa wote upeweumakini mkubwa.

Pia ameahidi kufikisha maombi ya Waziri wa Nishati ikiwa nipamoja na kuondolewa vikwazo vya upataji wa fedha kwa nchi zinazoendeleaikiwemo Tanzania kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki Moon.
Posted by MROKI On Friday, April 20, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo