Nafasi Ya Matangazo

April 02, 2012

Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT), mkoa wa Kagera ambalo ni tawi la ALAT taifa, inaandaa kongamano la mwaka 2012 pamoja na maonesho litakalofanyika kuanzia tarehe 4 Mei ,hadi 5 Mei, 2012 katika hoteli ya Kolping mjini Bukoba.

ALAT (M) Kagera kupitia wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ilimuomba Balozi Dk. Richard Sezibera, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa Mgeni Rasmi, tunayofuraha kubwa sana kwamba amekubali ombi letu kufungulia Kongamano hilo. Ni stahiki hapa kutoa shukurani zetu za dhati kwa ushirikiano tuliopewa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stergomena Tax, ambako tulipitisha ombi letu. Kwa hiyo tumeona sasa ni wakati muafaka kuanza kuihamasisha jamii ili kulifahamu jambo hilo.

Kutokana na umuhimu wa mkutano huo kwa maendeleo ya ki-uchumi na ki-jamii ya mkoa wa Kagera tumelipa jambo hili umuhimu mkubwa na ndiyo maana Mwenyekiti wa ALAT (M) Kagera  na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Dk. Anatory J. Amani akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, tuwe na mkutano na ninyi (Press conference) hii leo, ili kuufahamisha umma wa watanzania juu ya tukio hilo kubwa na muhimu sana lililoko mbele yetu.

 Mkoa wa Kagera ndio unaopakana nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mkoa wa Kagera unapakana na Rwanda na Burundi upande wa Magharibi hadi Kusini Magharibi, Uganda upande wa Kaskazini na kwa kupitia majini ndani ya Ziwa Viktoria unapakana na Kenya upande wa kaskazini Mashariki. Mkoa wa Kagera umo kwenye eneo la Bonde la Ziwa Viktoria ambalo ni eneo muhimu sana kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, likiwa ni lenye idadi kubwa ya watu na rasilimali nyingi sana na hivyo rasilimali ya pamoja ya nchi hizo kiasi cha kupelekea eneo hilo kutambuliwa kuwa ndilo eneo mahsusi la ukuzaji wa uchumi ambalo nchi wanachama zitaliendeleza kwa pamoja.
Ni kwa sababu hizo tumeamua Kongamano litafanyika kwa kauli mbiu “Mkoa wa Kagera ndiyo kiunganishi cha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki; Tuzitambue fursa za Soko la Pamoja ili tuzichangamkie”. Ni ukweli ulio dhahiri kuwa mkoa wa Kagera una kila sababu ya kuzitambua na kuzichangamkia fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC – Common Market). Kwa hiyo ili kuzijadili fursa na changamoto za Tanzania katika Soko la Pamoja kwa kuutumia mkoa wa Kagera kutokana na nafasi ya mkoa kijiografia katika jumuiya ya Afrika Mashariki, mada zifuatazo zitajadiliwa:

1.   Fursa na changamoto za ki-uchumi za mkoa wa Kagera, ambayo itawasilishwa RAS wa Kagera;

2.   Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki likielezewa katika lugha nyepesi, ambayo itawsilishwa na Sektretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wenyewe;

3.   Fursa na changamoto katika kilimo ndani ya mkoa wa Kagera, tumeomba iwasilishwe na  wizara ya kilimo, chakula na ushirika;

4.   Fursa na changamoto za biashara na nchi tunazopakana nazo, tumeomba iwasilishwe na wizara ya biashara na viwanda;

5.   Fursa na changamoto za uvuvi ndani ya mkoa wa Kagera katika Ziwa Victoria na ufugaju wa samaki, tumeomba iwasilishwe na wizara ya mifugo na uvuvi;

6.   Fursa na changamoto za kusisimua utalii katika mkoa wa Kagera, tumeomba iwasilishwe na wizara ya maliasili na utalii;
Posted by MROKI On Monday, April 02, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo