Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiongozana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro,Sista Dennis wakati alipofika shuleni hapo na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo,ambapo aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidi ili waweze kuwa viongozi wa baadaye.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mmoja wa Walimu wa Shule ya Mtakatifu Ann's iliopo Mkoani Morogoro,Sista Martha (kushoto) wakati akiwasili shuleni hapo.Kulia ni Mke wa Mh. Lowassa,Mama Regina Lowassa na wa pili kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo,Sista Dennis.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's iliopo Mkoani Morogoro wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha Mh. Waziri Mkuu Mstaafu.
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro.
Waziri Mkuu mstaafu,Mh. Edward Lowassa pamoja na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwa katika picha ya pamoja na Walimu wa Shule ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro.




0 comments:
Post a Comment