Watuhumiwa wa kesi ya kuvua samaki kinyume cha sheria eneo la Tanzania katika Bahari ya Hindi kwa kutumia meli ya uvuvi,Nahodha Hsui Chin Tai (kushoto) na Wakala, Zhao Hinguin wakiwa ndani ya Mahakama Kuu (Kitengo cha Biashara),Dar es Salaam leo, baada ya kuhukumiwa kwenda jela miaka 20 na 10 au kulipa faini ya sh.bilioni 1 na bilioni 20.
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewahukumu kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini ya Sh bilioni 21 raia wawili wa China waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uvuvi haramu katika Ukanda wa Kiuchumi wa Tanzania (EEZ) na kuwaachia huru wengine watatu.
Aidha, samaki waliokutwa kwenye meli hiyo hawatahusika na amri yoyote ya Mahakama hiyo kwa sababu Serikali ilishawagawa bure katika taasisi mbali mbali.
Pamoja na adhabu hiyo, Mahakama pia iliamuru meli ya Tawaliq I ambayo ilitumika kwa uvuvi huo haramu itaifishwe na Serikali ya Tanzania, kwa sababu ilikuwa ikifanya shughuli hiyo ya uvuvi kwa majina mbalimbali.
Baadhi ya magazeti likiwamo hili, jana yalichapisha picha ya meli hiyo ambayo inaonekana kuanza kuzama karibu na bandari ya Dar es Salaam.
Akisoma hukumu hiyo jana, Jaji wa Mahakama Kuu, Augustine Mwarija alisema anawatia hatiani mshitakiwa wa kwanza ambaye ni nahodha wa meli, Hsu Chin Tai na wa saba, Zhao Hanquing ambaye ni wakala wa meli.
“Nimezingatia kuwa meli hiyo imefanya shughuli za uvuvi katika majina mbalimbali tofauti na kwa vibali tofauti, mwenendo huo unaonesha kuwa haitambuliki, hivyo naona itaifishwe,” alisema Jaji Mwarija.
Jaji lisema sheria inayohusiana na uvuvi katika bahari kuu eneo la kiuchumi (EEZ) kifungu cha 18(1) inaelekeza kwamba kosa likithibitishwa, vifaa vilivyotumika hutaifishwa. Katika mashitaka ya kwanza ya kufanya shughuli za uvuvi katika Ukanda wa Bahari Kuu ya Tanzania bila leseni ambayo yanawakabili washitakiwa wote, Jaji aliwahukumu kulipa faini ya Sh bilioni moja kila mmoja au kifungo cha miaka 20 jela.
Jaji Mwarija alisema ni dhahiri meli hiyo ilifanya uvuvi katika bahari ya Hindi ukanda wa Tanzania na upande wa Jamhuri ulithibitisha kuwa uvuvi huo ulifanywa bila kibali chochote na kwamba samaki waliokutwa kwenye meli walikuwa wamevuliwa muda mfupi kabla ya kukamatwa.
Alisema ni kazi ya nahodha kuhakikisha vibali vya shughuli za majini wanavyo na ni halisi, hata hivyo alisema baadhi ya washitakiwa katika maelezo yao ya onyo, walikiri kufanya uvuvi. Alisema meli hiyo haikuwa na leseni na walipokamatwa, washitakiwa walitoa leseni iliyokwisha muda, hata hivyo ilikuwa imeandikwa jina ambalo si la meli hiyo, Tawaliq 2, na walidai kwamba meli hiyo ilikuwa inapita kwenda Mombasa, Kenya.
“Wazee wa Baraza katika maoni yao, pia waliwaona mshitakiwa wa kwanza (nahodha) na wa saba (wakala) wana hatia, nahodha ndiye anatakiwa kuhusika na vibali kabla ya kuanza kuvua, hivyo nawatia hatiani katika mashitaka ya kwanza,” alisema Jaji Mwarija.
Katika mashitaka ya pili ya kuchafua mazingira ya bahari kwa uchafu wa samaki na mafuta ya meli, yaliyomkabili nahodha peke yake, Jaji alisema ni wazi kosa hilo lilitendwa, kwa sababu samaki walikutwa kwenye meli bila uchafu ikionesha kuwa ulitupwa baharini.
Alisema mshitakiwa wa kwanza (nahodha) ana wajibu wa kuhakikisha kwamba sheria zinafuatwa, hivyo akamtia hatiani katika mashitaka hayo ambapo adhabu yake baadaye aliitaja kuwa ni faini ya Sh bilioni 20 au kifungo cha miaka 10 jela na kufafanua kuwa adhabu za kifungo zinakwenda sambamba.
Kabla ya kutamka adhabu hizo, Wakili Mkuu wa Serikali, Biswalo Muganga, aliiomba Mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho, kwa sababu jamii na nchi imepata hasara kutokana na makosa waliyofanya washitakiwa na kuiomba Mahakama itaifishe meli kama sheria inavyotamka.
Akitoa utetezi wa washitakiwa ili wapunguziwe adhabu, Wakili Ibrahim Bendera, aliiomba Mahakama katika kutoa adhabu izingatie urafiki kati ya Tanzania na China na pia muda ambao washitakiwa wamekaa mahabusu (miaka mitatu) kwamba tayari ni fundisho kwao na hivyo hapana haja ya adhabu nyingine.
Aidha, alisema ombi la meli kutaifishwa lililotolewa na Wakili wa Serikali, lisikubaliwe na badala yake meli itathminiwe na kisha mmiliki alipe gharama yake, ainunue ili Serikali iepuke mzigo wa kuitengeneza.
Washitakiwa 31 waliachiwa huru Julai mwaka jana baada ya kusota mahabusu kwa miaka miwili na miezi minne, baada ya kubainiwa na Mahakama hiyo kwamba hawakuwa na kesi ya kujibu.
Mshitakiwa raia wa Kenya alifia mahabusu baada ya kuugua kwa muda mrefu. Walioachiwa jana ni mshitakiwa wa tisa, Hsu Sheng Pao na wahandisi wawili wa meli hiyo, Cai Dong Li na Chen Rui Hai.
Source:Habarileo online

0 comments:
Post a Comment