Nafasi Ya Matangazo

February 12, 2012

Mwanamuzi, Muigizaji na Mwanamitindo mzaliwa wa Marekani Whitney Elizabeth Houston (August 9, 1963 – February 11, 2012) amefariki Dunia hii leo.

Taarifa zinadai kuwa Houston amekutwa amekufa katika chumba cha Hoteli alimokuwa amelala na madaktari waliofika katika Hoteli hiyo ya Beverly Hills walithibitisha kifo hicho.

Wakati ambapo bado chanzo cha Kifo chake hakijajulikana, Ofisa Habari wake Kristen Foster amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kusikitisha.

Houston alipangwa kuhudhuria sherehe za utoaji tuzo za awali Grammy za muziki na tayari alishaanza mazoezi wiki hii kwaajili ya tukio hilo. Clive Davis, aliomba muda wa watu kuwa kimya na kudai kuwa watatenga usiku huo kuwa maalum kwaajili ua Houston.

Rais wa Recording Academy Neil Portnow amesema sherehe za Grammy zitakazo fanyika Jumapili zitahusisha pia kitu maalum ambacho kitakuwa ni shukrani kwa Mwimbaji huyo ikiwa ni pamoja na show maalum kutoka kwa Jennifer Hudson. "Kitu kizuru kutoka kwa Whitney ni mchango wake ambao ameuacha kwetu."

"Whitney siku zote alikuwa ni mwenye tabasamu kali ambalo daima lilitupa nguvu” alisema Diddy, ambaye pia alihudhuria katika mkutano wa awali wa Tuzo za Grammy. "Whitney Houston alikuwa na sauti nzuri sana katika dunia hii. Hakika tumempoteza Malaika."

Whitney Houston, ni mtoto wa Muimbaji wa Nyimbo za Injili Cissy Houston na Binamu wa Mwimbaji Dionne Warwick amekuwa mshindi mara sita wa tuzo za  GRAMMY.

Atakumbukwa sana kwa vibao vyake matata vilivyopata kutamba miaka ya 80 na 90 vya "The Greatest Love of All," "I Will Always Love You," "How Will I Know" na  "I'm Every Woman." Pia katika uigizaji ambako pia alikuwa na kipaji hicho na alishiriki katika Filamu za The Bodyguard na Waiting to Exhale.

Mbali na tuzo za Grammy pia Houston alishinda mara mbili tuzo za EMMY na mshindi mara 22 wa Tuzo za American Music.

 Marehemu aliwahi kuolewa na na Mwimbaji wa R&B, Bobby Brown kati ya mwaka 1992 na 2007, ambapo wawili hao walijaaliwa kupata Mtoto mmoja wa kike, Bobbi Kristina Brown, aliyezaliwa mwaka 1993. Pia wanandoa hao walikuwa wakishiriki katika mfululizo wa vipindi vya Televisheni vya Being Bobby Brown in 2005.

Watu mbalimbali wametuma salkamu za rambi rambi wakiwapo wanamuziki wenake Mariah Carey aliyebainisha kuwa Houston alikuwa ni mshirika wake wa karibu na katu hato msahau maishani mwake na kifo chake ni pigo kubwa na amewapa pole wanafamilia yake, na mashabiki na wapenzi wake popote duniani.

Blogu hii pia kwa niaba ya wadau wote inatoa pole kwa wote waliofikwa na msiba huu.
Posted by MROKI On Sunday, February 12, 2012 1 comment

1 comment:

  1. R.I.P Whitney Houston. we will always Remember you!!

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo