Mh. Mohammed Raza
Na Khadija Khamis –Zahira Bilali –MAELEZO
Tume ya Uchaguzi Zanzibar imemtangaza rasmi Mohamed Raza Hassanali Mohamadali kuwa Mwakilishi halali wa Jimbo la Uzini kwa kushinda asilimia 91.1 sawa na kura 5377.
Matokeo hayo yametolewa na Afisa Msimamizi Uchaguzi wa Wilaya ya Kati Mussa Ali Juma huko katika Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kati Unguja. Alisema kuwa zoezi la Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Uzini ulikwenda vizuri mpaka kufikia katua ya matokeo.Alisema kuwa Vyama vilivyoshiriki katika zoezi hilo vilikuwa jumla ya vyama vitano ndivyo vilivyoweza kusimamisha wagombea wake navyo ni AFP,CCM,CHADEMA .CUF na TADEA .
Matokeo ya uchaguzi huwo ulikuwa kama ifuatavyo kwa upande wa CCM mgombea wake Mohamedraza alipata kura 5377, Rashid Yussuf Mchenga wa AFP alipata kura 08 Khamis Khatib Vuai wa TADEA alipata kura 14 Salma Hussein Zaral wa CUF amepata kura 223,na Ali Mbaruku Mshimba wa CHADEMA alipata 281 .
Alieleza kuwa jumla ya wananchi waliondikishwa katika uchaguzi huo ni 8743 waliyojitokeza kupiga kura 5931 kura halali 5903na kura zilizoharibika 28 .Nae Mgombea wa CCM aliebukia kuwa mshindi wa uchaguzi huo aliishukuru Tume ya Uchaguzi kwa kuendesha zoezi hilo kwa ufanisi .
Pia aliwahidi wananchi wake wa jimbo hilo kuwa atawatumikia bila ya kujali ubaguzi na itikadi za kisiasa na kuwaletea maendeleo kwa vitendo kama ilani ya chama chake inavyoeleza .Zoezi hilo la uchaguzi limefanyika kutokana na kufariki kwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Marehemu Mussa Khamis Silima .
0 comments:
Post a Comment