Mhuduma wa Stationari Magomeni aibuka mshindi wa mlioni 50 ya Airtel MZUKA Mshindi wa pili wa million 50 katika promosheni ya Mzuka wa Airtel apatikana.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania Jana iliendesha draw kubwa ya pili ya kutafuta mshindi wa milioni 50/TZS iliyofanyika jana usiku Majira ya saa mija na nusu na kurushwa live katika kituo cha television cha ITV na kushuhudiwa na watanzania wengi ambapo Bi Halima Omary Issa mkazi wa Magomeni Makanya aliibuka mshindi wa kitita hicho cha shilling million 50 pesa tasilimu.
Bi Halima Omary mwenye umri wa miaka 26 aliyeajiriwa kama mfanyakazi wa stationary alisikika kuwa mwenye furaha iliyozidi kifani pale alipopigiwa simu na Meneja uhusiano wa kampuni ya Airtel Bw Jackson
Mmbando na kupewa habari njema ya kuwa mshindi wa pili wa droo kubwa na kujishindia million 50 pesa taslimu.
Katika maojiano na mshindi huyo yaliyofanyika kupitia televisheni ya ITV live bi Halima Omari alisikika akisema “namshukuru sana mungu yani sewezi kuamini nilishiki sana promosheni hii na nashukuru sana kuibuka mshindi katika promosheni ya hii ya Airtel” Akiongea kwa niaba ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel meneja.
Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando “kupitia promosheni hii kabambe tayari tumempata mshindi wetu wa droo kubwa yapili ya milioni 50 TZS ya MZUKA lakini bado tumebaki na zawadi nyingi za simu mpya za kisasa za sumsung tablet pamoja na muda wa maongezi na pia mwisho wa mwezi wa pili tutampata mshindi wa droo ya tatu wa milioni 50/-TZS ya promosheni hii ya MZUKA” Pia alitumia nafasi hiyo kuwashukuru watanzania na wateja wa Airtel kwa kuendelea kutumia huduma za Airtel na kushiriki katika promosheni
hiyo, Promosheni ya Mzuka inaendeshwa na Airtel kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo ambapo ilizinduliwa rasmi mwishoni mwa mawka jana desemba hadi mwishoni mwa februari mwaka huu 2012.
Zawadi kabambe wanazojishindia wateja kila siku ni pamoja na simu aina ya Samsung, Muda wa maongezi, wakati washindi wa wiki wanajishindia Samsung ipad, na washindi wa kila mwenzi pesa taslimu shilling million
50 Promosheni ya mzuka wa Airtel bado inaendelea hadi mwisho wa mwenzi wa februari ambapo zawadi mbalimbali zinaendelea kutolea na droo kubwa ya mshindi wa tatu itachezeshwa mwishoni mwa mwenzi huu.
Kujiunga ni bure tuma ujumbe wenye neno “Mzuka” kwenda namba “15565” na ujipatie nafasi ya kuibuka kuwa moja kati ya washindi.




0 comments:
Post a Comment