Nafasi Ya Matangazo

January 23, 2012

 Maharusi Darius Mkiza na Alfredina Felix wakiwa na furaha baada ya kufunga ndoa yao takatifu Mwishoni mwa wiki katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam na baadae kufuatiwa na tafrija kubwa iliyofanyika katika ukumbi wa Holland Msimbazi Center jijini Dar es Salaam.
 Bi Harusi akiwa na wapambe wake
 wapambe wakiwa katika picha yao ya pekee...
 2012 bi harusi ndo anapaswa kumbeba Mwanaume na hapa Alfredina akitimiza hilo kwa mbinde ...lakini hapo chini ndo hivyo mambo yalimshinda na wakaenda mrama.
 Darius akimuimbia wimbo Mkewe kipenzi...hakika ilikuwa ni siku ya furaha sana.
 Ngoma za asili zilikuwepo kutoka huko huko Bukoba...
 Mambo ya kwaito yalinyanyua umati wa watu ukumbini hapo.
Baadhi ya waalikwa ambao ni Walimu na wanafunzi wenzake na Bwana Harusi katika PHD wakiwa ukumbini
 Wazazi wa bawana Harusi wakifuatilia tafrija hiyo.
 Wazazi wa Bi Harusi nao wakifuatilia tafrija hiyo
 Kamati ya Maandalizi ambayo iliongozwa na Mwenyekiti Mhandisi Dk. Pancras Bujulu (kushoto walio simama) ilifanya kazi nzuri.
 Walikwa wakiwa ukumbini
 Darius ni Mwana habari hapa ni wadau wa habari ambao pia alisoma nao wakiongozwa na Freddy Maro kushoto.
 Wanafunzi wa Darius pale SAUT Dar es Salaam walifika kumpa shavu
 Licha ya kuwa wapo katika game la habari kwa muda mrefu lakini sasa wapo shule tena kujifua Anastazia Anyimike akifuatiwa na Fatma Almas Nyangasa nao walikuwepo kutoka SAUT Dar es Salaam
 Wanafunzi walikuwa ni wengi kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Mwanza tawi la Dar es Salaam.
 Mambo ya Msosi yalikuwa balaa hadi senene walikuwepo.
 Maharusi Darius na Alfredina wakila pozi mbele ya Camera ya MD Digital Company kampuni ambayo ilipewa jukumu la kuchukua kumbukumbu katika harusi hii.
Hapa ndo ilikuwa katika kuwekana alama na ishara ya kumbukumkbu ya ndoa yao. Bi Harusi Alfredina akimvisha pete Bwana Harusi Darius.
Posted by MROKI On Monday, January 23, 2012 4 comments

4 comments:

  1. dah! safi sana mungu awabariki katika ndoa yenu!!

    ReplyDelete
  2. Hongereni sana Darius na Alfredina kwa kufunga ndoa. Mungu awatunze na kuwapa maisha yenye furaha na amani.

    ReplyDelete
  3. Hongera darius.

    ReplyDelete
  4. Mungu awabariki na awape maisha ya furaha na amani telee.Hongera sana

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo