Nafasi Ya Matangazo

January 17, 2012

Zantel ambayo ni kampuni Tanzu ya ya Etisalat Group  na ambayo ni kampuni ya simu selula yenye ubunifu mkubwa nchini Tanzania  inayofuraha kutangaza kuwa  imemteua Bw. Brian Karokola  kuwa Mkurugenzi wake mpya wa Masoko pamoja na Bw. Deo Kwivukwa  kuwa Mkuu wa Idara ya Usambazaji na Mauzo kuanzia Januari 02, 2012.

 Jukumu jipya la Bw. Karokola  kama Mkurugenzi wa Masoko  litakuwa ni kusimamia programu ya mikakati ya mipango ya  masoko, mawasiliano ya kampuni kwa kuangalia  mtiririko wa mapato ya rejareja  na kubuni mipango mipya. Nafasi hiyo ni muhimu katika kuendelea  kukua kwa bidhaa za Zantel  pamoja na  soko  lake nchini Tanzania.

 Ofisa Mkuu wa Biashara wa Zantel, Ahmed Mokhles akiidhinisha  uteuzi huo alisema kwamba Zantel ni mwajiri wa kuchaguliwa na Watanzania  na chimbuko la kukuza utaalamu  wa ndani.

“Ninayo furaha kuwatangaza uteuzi wa Bw. Karokola  kama Mkurugenzi wa Masoko na kuifanya Zantel  kuongoza  miongoni mwa waendeshaji wa  mitandao ya simu selula kwa kuteua mzawa kuongoza kitengo chake cha masoko. Hili lipo kwenye majukumu ya Etisalat Group katika kuwekeza kwenye wataalamu wa ndani”, alisema Mokhles.

 Brian Karokola ana Shahada  ya Uzamili kwenye Masoko (MBA) na hivi karibuni alimaliza  programu ya miezi 12 ya HiPo ambayo inajumuisha programu ya uongozi kibiashara kazini  kwenye mawasiliano ya simu inayotolewa kwa ubia  kati ya Etisalat Academy  kwenye Falme za Kiarabu (UAE) na Skuli ya Biashara ya Harvard ya  Marekani.   

 Deo Kwivukwa kwa upande wake kama Mkuu wa Kitengo na mauzo  jukumu lake litakuwa ni kuangalia  usambazaji, timu ya mauzo  na kusimamia mwenendo wa usambazaji  nchini hali kadhalika kuwezesha na kupanua bidhaa za Zantel zisambae nchini kote.

Kabla ya uteuzi wake  alikuwa ni  msimamizi wa kitengo cha Zantel Own Manager  kinachoshughulikia maduka na  vituo vya huduma kwa  wateja . Ana Shahada ya Uzamili kwenye  Masoko  akiwa amejikita kwenye  masuala yanayoliweka soko kwenye hali mbaya (MBA venturing in Marketing) .

Posted by MROKI On Tuesday, January 17, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo