Mchezaji Amir Hamad wa Zanzibar Heroers akimtoka mchezaji wa timu ya Somalia Kassim Ali Mursal wakati timu hizo zilipopepetana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam katika michuano ya kombe la TUSKER CHALLENGE CUP 2011, Timu ya Zanzibar Heroers imeifunga Somalia magoli 3-0.
Mchezaji wa timu ya Somalia Abdi Azizi akichuana na mchezaji wa timu ya Zanzibar Heroers Juma Othman wakati wa mchezo wao wa kuwania kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP kwenye uwanja wa Taifa leo.
Khalid Ali Maursal wa timu ya Somalia akiruka juu kuokoa mashabulizi kutoka kwa washabuliajiwa timu ya Zanzibar Heroers kwenye uwanja wa Taifa.
Amir Hamad wa Zanzibar Heroers na Kassim Ali Mursal wa Somalia wakichuana vikali wakati wa mchezo wao uliofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam katika mwendelezo wa michuano ya TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP.
Simeon Masaba wa timu ya taifa ya Uganda The Cranes akimtoka mmoja wa mabeki wa timu ya Burundi katika mchezo wa kuwania kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 uliomaliziki jioni hii kwenye uwanja wa Tafa jijini Dar es salaam, Katika mchezo huo timu ya Burundi imeifunga The Cranes goli 1-0.
0 comments:
Post a Comment