Nafasi Ya Matangazo

December 01, 2011

Revocatus Ngowi (kushoto) na Daniel Ngowi wakiwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro walipoipandisha bendera ya Taifa ikiwa ni kilele cha Kampeni ya Kilimanjaro Jivunie uTanzania iliyokuwa ikiendeshwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager illi kusherekea miaka 50 ya Uhuru.

HATIMAYE Kampeni ya Kili Jivunie uTanzania iliyokuwa ikiendeshwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager imefikia kilele chake baada ya bendera ya Taifa kupandishwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Bendera hiyo ilipandishwa Jumapili Novemba 27 na vijana watatu mahiri ambao ni watalamu katika masuala ya upandaji mlima na uongozaji wa watalii walitumia saa 20 kupanda mlima huo na kushuka.

Vijana waliofanya kitendo hicho cha historia cha kupandisha bendera ni Daniel Ngowi, Revocatus Ngowi na Aloyce Joseph ambao ni maarufu kwa upandaji wa mlima huo na pia uongozaji wa watalii.

Bendera hiyo ilipandishwa baada ya kumalizika kwa mbio za bendera zenye rangi nne za bendera ya taifa kutoka mikoa minne na baadaye kuunganishwa Moshi na kupatikana bendera moja iliyopandeishwa katika Mlima Kilimanjaro.

Akiwapokea vijana hao Jumanne katika geti la Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro, Wilayani Marangu, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe aliwapongeza kwa kutimiza malengo ya kampeni ya Jivunie uTanzania.

“Nawapongeza sana kwa kuonesha ushujaa na pia kuandika historia kwani miaka 50 ya Uhuru haitajirudia tena…ni jambo la kujivunia sana,” alisema.

Akizungumza mara baada ya kushuka, Daniel Ngowi alisema, “Najiskia fahari sana kuweza kufanya kitendo hiki cha historia ambacho sikuwahi kufikiri ningefanya maishani.” 

Naye Revocatus Ngowi alisema kitendo kilichofanywa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia ya Kilimanjaro premium Lager cha kupandisha bendera ya taifa katika mlima Kilimanjaro ni cha historia ya kipekee na kuwa yeye alifarajika sana kupata fusa ya kupandisha bendera hiyo.

Aloyce Ngowi alisema, “Tumechukua saa 20 kupandisha bendera hii katika MLima Kilimanjaro pamoja na changamoto zote za hali ya hewa na kilichotufanya tujitume ni umuhimu wa shughuli hii na kumbukumbu yake katika historia ya nchi yetu.”

Awali kabla hawajaondoka vijana hao waliagwa na Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye katika lango la Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro huku akiwaasa Watanzania wawe na mazoea ya kujivunia Utanzania wao na kusema ujumbe ulioletwa na Kampeni hii ya Kilimanjaro ulikuwa na maana kubwa sana kwa watanzania.

Kampeni hii ilizinduliwa July 5, mwaka huu kwa lengo la kusherekea miaka 50 ya Uhuru na kuwakumbusha Watanzania kujivnia mafanikio yaliyopatikana hadi sasa.
Posted by MROKI On Thursday, December 01, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo