Abel Loshilaa Motika a.k.a Mr Ebbo, atakumbukwa sana kwa nyimbo zake alizoimba kwa maahadhi ya matamshi ya Jamii ya Wafugaji kutoka Mkoani Arusha Wamasai Ambako yeye ni asili yake.
Miongoni mwa nyimbo hizo zilizo jizolea umaarufu mkubwa miaka ya 2002-2004 ni pamoja na wimbo wa Mi Mmasai, Kamongo, Unisamehe, Fahari Yako, Njaa inauma, Bado Kusungumsiwa.
Hakika kila aliyezisikia nyimbo hizi zikipigwa redioni au zikichezwa katika Klabu na kumbi mbalimbali za starehe walivutiwa sana nazo na kiasi cha baadhi ya watu kutokana na upenzi wao katika nyimbo hizo walipewa majina kama lile la KAMONGO.
Binafsi nilipewa jina la Kamongo pale Kijitonyama CCM katika Bar Ambayo nilipenda sana kufika kila jioni na nifikapo wimbo huo ulichezwa na kila mtu kujua Kamongo ameingia.
Nilianza kumfahamu Mr Ebbo mwaka 2002, Nikiwa Mwandishi wa Habari pale The Guardian Ltd, na mara kadhaa nilifanya nae mahojiano kuhusiana na Nyimbo zake.
Niliwahi kuandika mashairi ya nyimbo zake hasa ule wa Mi Mmsaai bwana, hakika ni wimbo mzuri na wakuvutia ambao kila mtanzania anapaswa kujivunia asili yake.
Motika aliyevuta pumzi yake ya kwanza katika dunia hii mnamo Mwezi 26, May 1974 na kushindwa tena kuvuta pumzi hiyo Desemba 2, 2011 kule kule alikozaliwa mkoani Arusha baada ya kuugua kwa muda.
Alipata elimu yake ya Msingi Kijenge na baade mwaka 1984 alihamia jijini Tanga katika shule ya Msingi Nguvumali na kisha kupata elimu yake ya Sekondari Juiya na kuhitimu 1992.
Mr. Abbo Alirudi Arusha mwaka 1993 na kubahatika kupata kazi kwenye night club ambapo alitumia mishahara yake kurekodi nyimbo ambazo hazikumpa mafanikio yeyote isipokuwa zilimuweka katika ramani ya muziki. Baada ya hapo alifanya kazi ya kuandaa matangazo ya biashara na vipindi vya redio kwenye studio iliyojulikana kama Supreme recording studios iliyopo mjini Arusha.
Kipindi hicho kilijulikana kama “Mambo gani haya” Alirekodi nyimbo kadhaa ambazo hazikumpa mafanikio yoyote kwa mara nyingine na hali hiyo ikamkatisha tamaa kabisa.
Baadae mwaka 1995 Alipata kazi ya kuuza nguo kwenye duka la JJ BLACK lililopo jijini Arusha. Mwaka 1999 Aliamua kurudi jijini Tanga na akafanikiwa kufunga ndoa na kubahatika kupata watoto wawili Ashley na baadaye Alicia. Alianza kazi ya uwakala wa kuuza magazeti mwaka 2000.
Kazi ambayo pia haikumletea mafanikio yeyote makubwa kama alivyokuwa anatarajia, baadaye mwaka 2001 akaanzisha biashara ya kuuza mchele kwa jumla ambayo pia haikuwa na mafanikio aliyoyatarajia. kipindi hicho chote alipokuwa Tanga alifahamiana na Wasanii wa Muziki wa Bongo Fleva,Professor J na Wagosi wa kaya, na wao pia walijua kuwa Mr. Ebbo ni Msanii asilia. Baadae alijiunga na chuo cha kozi za computer jijini tanga.
Wagosi waliporekodi wimbo wao wa Tanga kunani ,Mr Ebbo alihamasika kurudi tena kwenye Muziki na ndipo alipoandika wimbo wa kwanza wa "Mimi Mmasai mwaka 2002". Wimbo huo ukatambulisha Album yake ya kwanza kisha wimbo wa “ Fahari yako “ Baadaye mwaka 2003 akafungua studio ( MOTIKA RECORDS) Ambayo ilifanikiwa kuwatambulisha wasanii kama, Danny Msimamo, Dr Leader, Mo-Kweli, na wengineo wengi , wote hawa aliwaproduce yeye mwenyewe. kama producer wa MOTIKA RECORDS.
Mwaka 2003 akarekodi Album yake ya pili iliyojulikana kwa jina la Bado Ijasungumiswa. Mwaka 2004 akarekodi Album yake ya tatu iliyoitwa Kazi gani. Mwaka 2005 akarekodi Album ya nne iliyoitwa Alibamu. Mwaka 2006 akarekodi Album ya tano inayoitwa Kamongo. Kamongo ndio albamu ya mwisho kwa uhai wake.

Katika Nyibo zote alizowahi kuimba Marehemu, Mr Ebbo, nilivutiwa nazo na leo nalazimika kuuzungumzia wimbo wake 1 tu ambao ni MI MMASAI.
Mr.Ebbo alitukumbusha kujivunia asili zetu kama yeye alivyojivunia Umasai wake ambao hienda baadhi yetu tunazikana asili zetu kwa namna moja au nyingine.
“Mi Mmasai bwana nasema mi Masai, ….Najivunia Mmasai …, Kabila pekee inayodumisha mila” hakina ni ukweli kabila pekee ambalo hadi hii leo linadumisha mila ni Kabila la Mmasai kutokana na Mavazi yao, tamaduni na hata makazi yao hakuna kabila ambalo hadi hii leo lipo kama wao.
Hivyo Watanzania hii leo tukiomboleza kifo cha Jasiri huyu Abel Loshilaa Motika kwa kuenzi utamaduni na kutamka hadharani kujivunia kwake asili yake, hatuna budi kujivunia na sisi asili zetu.
Hii itapendeza sana Mluguru akijivunia kuwa Mluguru, Mchaga, Mpare, Makonde, Msukuma, Mpogoro, Mzanaki, Mtindiga, Msandawe kila mmoja kwa nafasi yake ajivunie asili yake na kudumisha mila ya na destruí za kwao.
Hivi unajisikia raha gani wewe Msimbe mtu akikuita we Mluguru na unakuwa mkali kuwa si mluguru, au Mgonja unapokana Upare wako?. Vipi nawe Msandawe au Mrangi ukane asili yako? Kuna raha yake ya kujivunia asili zetu kakma vile ambavyo Mr Ebbo alitukumbusha mika cada iliyopita lakini hatukuuchukulia maanani wimbo ule na kuona ni burudani tu.
Kama alivyo wahi kusema baba wa Taifa hili Mwalimu JK Nyerere wakati akikemea kujitenga kwa Tanzania bara nba Zanzibar kuwa dhambi ya kujitenga iklituingia haita ishia hapo bali itazidi hata huko Zanzibar patatokea Muunguja na Mpemba.
Hili la kukana asili zetu za mababu na mabibi likifanyika hutokea lile la kukana hata uraia wako. Yes yupo mtu ambaye akisha ukana Uluguru wake mwisho wa siku atasema mimi ni Black America!! Maana kabila lake amesha likana unadhani ata asili wapi kama si huko kwa wakata mkonge ambao miongoni mwao asili zao ni África shahidi Obama ambaye asili yake ni Kenya.
Mungu aipumzishe roho ya marehemu Abbel Loshilaa Motika “Mr. Abbo” mahala pema peponi na aitie nguvu familia yake, ndugu jama na marafiki popote pale na wapenzi wake wote wa muziki.
0 comments:
Post a Comment