Nafasi Ya Matangazo

December 23, 2011

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mmoja kati ya wananchi waliohifadhiwa katika Kambi ya Shule ya Sekondari ya Azania, waliookolewa katika maeneo yaliyojaa maji kutokana na mvua zilizonyesha jijini Dar es Salaam kuanzia majuzi, wakati Makamu alipofika katika Kambi hiyo leo Desemba 23, kwa ajili ya kuwapa pole waathirika hao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Bi. Monica Luis, Mkazi wa Jangwani aliyeathirika na mafuriko ya Mvua kubwa iliyonyesha jijini kuanzia majuzi, wakati makamu alipotembelea katika Kambi ya Shule ya Sekondari Azania jijini Dar es Salaam leo Desemba 23, kwa ajili ya kuwapa pole waathirika wa mafuriko hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wananchi waliohifadhiwa katika Klabu ya timu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam, wakati alipowatembelea kuwapa pole wananchi hao walioathirika na mafuriko ya Mvua kubwa zilizonyesha jijini kuanzia majuzi. Makamu alifanya ziara hiyo ya kutembelea baadhi ya kambi za waathirika leo Desemba 23, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo ya jinsi maji yalivyokuwa yamejaa wakati wa mvua kubwa iliyosababisha mafuriko, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick (kulia), wakati alipotembelea kuwapa pole wananchi waliokuwa wamehifhadhiwa katika Klabu ya Yanga, iliyopo Jangwani leo Desemba 23,2011.
Posted by MROKI On Friday, December 23, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo