Nafasi Ya Matangazo

December 24, 2011

Kutoka kulia ni Mtangazaji wa kipindi cha Michezo Clouds FM/TV Shafii Dauda alipokuwa akiwafanyia mahojiano mafupi kwa wachezaji wa mpira wa miguu wa zamani ambao wameathirika na mafuriko yaliyotokea hivi karibuni,anayefuatia ni Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mh.Idd Azan,Mwanamtwa Kihwelu (aliyewahi kuichezea timu ya Simba na Yanga),Robert Damian (mwenye kofia-Simba),Mtangazaji wa kipindi cha Michezo Clouds Fm/TV Ibrahim Masoud,Dua Said (Small Simba & Simba S.C),Maalim Salehe a.k.a Romario (Yanga),Shaaban Ramadhan (Simba,Yanga,Mlandege & Mtibwa) pamoja na Mke wa Marehemu Nico Bambaga ambaye alikutwa akijishughulisha kutoa tope zito lililokuwa limenasa kwenye nyumba yake aliyokuwa akiishi na familia yake.Wachezaji wote hao akiwemo Peter Manyika ambaye hayupo pichani nyumba zao zote zimeathiriwa vibaya na mafuriko.
Aliyewahi kuwa mchezaji wa timu ya Yanga na Simba,Mwanamtwa Kihwelu akifafanua namna adha ya mafuriko ilivyowakumba,mbele ya Mbunge wa jimbo la Kinondoni,Mh Idd Azan,wakati kampuni ya Clouds Media Group ilipokwenda kutoa misaada kwa waathirika na pia kujionea maeneo mbalimbali yalivyoharibiwa na mafuriko hayo,mapema leo mchana jijini Dar,pichani kati ni mmoja wa Wakurugenzi wa Clouds Media Group,Bw.Ruge Mutahaba ambaye pia aliongozana na baadhi ya wafanyakazi wa kampun hiyo mpaka eneo hilo la tukio na kujionea hali halisi.
Mmoja wa wachezaji waliowahi kuwika miaka kadhaa nyuma,Dua Said aliyekuwa akiichezea timu ya Small Simba na hata Simba S.C akionesha nyumba yake ilivyoathiriwa na mafuriko yaliyotokea hivi karibuni jijini Dar,Camera ya Jiachie ilitinga mpaka ndani ya nyumba hiyo na kujionea hali halisi,ama kwa hakika hakuna kilichobaki,vitu vingi viliondoka na maji na ndani kubakia tope zito,ambalo mpaka sasa Dua anasema hajui aanzie wapi kuliondoa.
 Mkurugenzi wa Biashara Clouds Media Group,Dada Sheba akitoa salamu za pole kwa Mbunge wa jimbo la Kinondoni,Mh Idd Azan kwa niaba ya baadhi ya Wananchi wake walioathiriwa na mafuriko yaliyotokea hivi karibuni jijini Dar na kusababisa madhahara makubwa,Aidha uongozi wa Clouds Media Group pia ulikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa Mh Idd Azan pichani kulia,mapema leo mchana kwenye kambi ya muda iliopo shule ya Msingi ya Lutihinda,iliyowekwa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akiwa ameambatana na baadhi ya wafanyakazi (hawapo pichani),akitoa maneno ya pole kwa waathirika wa mafuriko pamoja na kuwaeleza misaada mbalimbali walioitoa,aidha Ruge amesema kuwa pamoja na kutoa msaada huo wa vyakula,nguo na mambo mengine,wataweka hema ambalo litahusika kwa ajili ya kutolea huduma ya kwanza na pia kuwahamasisha wanajamii mbalimbali watakaoguswa kujitolea kuleta madawa mbalimbali kwa ajili ya huduma ya kwanza,kwani eneo hilo lina mkusanyiko mkubwa wa watu,hivyo mambo ya magonjwa mbalimbali ikiwemo ya mlipuko yanaweza kutokea. 
Mbunge wa jimbo la Kinondoni,Idd Azan akizungumza na baadhi ya wananchi waliothirika na mafuriko kwenye kambi yao ya muda iliyopo shule ya msingi ya Lutihinda,Kigogo jijini Dar,ambapo kampuni ya Clouds Media Group ilifika eneo hilo na kutoa msaada wa vitu mbalimbali,ambavyo vilipokelewa na Mbunge huyo,Idd Azan
Pichani juu na chini ni wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Dogo Ditto pamoja na AT wakiwaimbia baadhi ya watoto walioko kwenye kambi ya muda ya waliothirika na mafuriko yaliyotokea hivi karibuni jijini Dar,kambi hiyo imewekwa kwenye shule ya msingi Lutihinda,kata ya Kigogo wilaya ya Kinondoni,ambapo kampuni ya Clouds Media Group ilikwenda kutoa msaa wa vitu mbalimbali ikiwemo maji,vyakula,magodoro pamoja na nguo,aidha kama vile haitoshi Clouds imeahidi kutoa msaada wa madawa mbalimbali na kuweka hema la huduma ya kwanza katika kambi hiyo,ambapo waathirika wamekusanyika eneo hilo kwa wingi lakini hakuna huduma yoyote ya kiafya.
Posted by MROKI On Saturday, December 24, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo