Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Bernald Membe akizungumza katika maazimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania katika wizara hiyo yaliyofanyika leo, kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja na kuhudhuriwa na wafanyakazi pamoja na mabalozi wastaafu mbalimbali.
Akizungumza katika maadhimisho hayo moja ya mambo aliyozungumzia ni kifo cha aliyekuwa rais wa Libya Marehemu Muamar Gaddafi, aliyeuawa na majeshi ya NTC jana nchini Libya, Membe amesema "Tanzania au watanzania hawawezi kufurahia kifo cha Muamar Gaddafi kama binadamu mwenye uhuru na haki ya kuishi kama binadamu mwingine, hata kama angekuwa na makosa".
Kuuawa kwa Gaddafi haimaanishi kwamba ndiyo kutakuwa kumepatikana amani ya kudumu nchini Libya, badala yake huenda kukawa na machafuko zadi kama ilivyo kwa nchi kama Tunisia, Misri na kwingineko ambako watawala wameondolewa madarakani kwa maandamano na mabavu.
Ameongeza kwamba leo Tanzania inaadhimisha miaka 50 kwa misingi aliyoiweka Baba wa taifa Mwalimu Julius K. Nyerere, misingi iliyotufanya kuwa huru, wamoja na wenye kuheshimiana na kupendana.
Mfanyakzi bora wa jumla katika wizara ya mambo ya nje Bw.Seif Kondo kulia kutoka kitengo cha habari akipokea cheti cha ufanya kazi bora kutoka kwa Waziri Bernald Membe.
Waziri Bernald Membe akimkabidhi cheti cha ufanyakazi bora Grace Mjuma Kaimu mkurugenzi Idara ya Mawasiliano ya Kikanda.
Waziri Bernald Membe wa tatu kutoka kulia akiwa amekaa meza kuu pamoja na mabalozi wastaafu walioshiriki katika maadhimisho hayo.
Kundi la THT kutoka jijini Dar es salaam likitumbuiza katika maadhimisho hayo.
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika maadhimisho hayo viwanja vya Mnazi Mmoja leo.
Wafanyakazi wa Wizara ya mambo ya nje wakishiriki katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania katika wizara hiyo.
Wafanyakazi wa Wizara ya mambo ya nje wakishiriki katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania katika wizara hiyo.
0 comments:
Post a Comment