Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara akimpatia kitabu cha taarifa ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara kwa Wizara hiyo leo nyumbani kwa Mjane wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake Butiama, mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara mara baada ya kumtembelea Mjane wa Mwalimu Nyerere, Mama Maria Nyerere kijijini kwake Butiama, mkoani Mara leo. Wengine katika picha ni Viongozi waandamizi wa Wizara hiyo, kulia hiyo ni mtoto wa Hayati Baba wa Taifa, Madaraka Nyerere.
Mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Charles Makongoro Nyerere akitoa historia ya makaburi ya wazazi wa mwalimu Julius Nyerere yaliyopo mwitongo, Butiama kwa Viongozi waandimizi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waliokwenda kumjulia hali Mama Maria Nyerere.
Mkuu wa mkoa wa Mara John Tupa(katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika banda la Idara ya Habari kuhusiana na maandalizi ya mbio za mwenge wa uhuru unaotarajia kuwashwa mkoani humo. Wa pili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Sihaba Nkinga na kwanza na kwanza kushoto ni kaimu Afisa Utamaduni na Michezo, Shekheadi Saidi. Wengine wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Clement Lujaji na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Karaine Kimaati.
Mama Maria Nyerere akiteta jambo na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara nje ya nyumba yake mara baada ya mazungumzo na Viongozi waandimizi wa Wizara hiyo. Kulia ni Naibu Katbu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Sihaba Nkinga.
Posted by MROKI
On Wednesday, October 12, 2011
2 comments
Kwanini hamuulizi watu majina yao? Huyo huyo "Madaraka Nyerere" anakuwaje tena "Makongoro Nyerere"?
ReplyDeletePoa Madaraka,tumekupata mkuu.Ex Bunge
ReplyDelete