Nafasi Ya Matangazo

October 25, 2011

 Uvuvi ni moja ya vitu ambavyo huwapatia watanzania walio wengi kipato na kuwezakluyamudu maisha yao ya kila siku katika maeneo mengi ya nchi ambayo yana mito, mabwawa, maziwa na bahari. Miongoni mwa mikoa ambayo imejaliwa kuwa na mabwawa makubwa na mito mingi ni Mkoa wa Morogoro. Mkoa huu unabwawa maarufu sana la Mindu lililopo kando kando ya barabara kuu ya Morogoro-Iringa-Mbeya na Zambia.
 Wakazi wa kijiji cha Mindu na maeneo yote jirani na hata mjini wamekuwa ama wakijishughuloisha na shughuli za Uvuvi katika bwawa hilo au kufanya biashara ya samaki. Pichani ni miongoni mwa wachuuzi wa samaki wakiangalia samaki waliotoka kuvuliwa muda si mrefu.
 Hapa ni biashara ikifanyika. Lakini uhifadhi wa mazingira katika mabwawa kama hili la Mindu ndio njia kuu ya kuwa na samaki wengi. Kiwango cgha samaki bwawani hapa kimepungua na upatikanaji kuwa mgumu. Bwawa kuwa na magugu na uvuvi wakutumia nyavu ndogo huenda ukawa ndio chanzo kikuu, ingawa wavuvi wanasema msimu wa maji kuingia kutokana na mvua ndio chanzo.
Wavuvi katika Bwawa hili wana umoja wao ambao mbali na mambo mengine wamejiwekea sheria za uhifadhi mazingira kama huu unaoonekana katika kibao hiki.
Posted by MROKI On Tuesday, October 25, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo