TUZO ZA KWANZA ZA UBUNIFU WA MAVAZI AFRIKA MASHARIKI NA KATI KUZINDULIWA LEO
MASHINDANO YA KWANZA YA UBUNIFU WA TISHETI KUFANYIKA TANZANIA
Swahili Fashion Week ni maonyesho makubwa yatakayohusisha Afrika mashariki na kati. Kwa mwaka wake wa nne sasa Swahili Fashion Week itafanyika NationalMuseum tarehe 10,11 na 12 Novemba 2011 Dar-es-salaam Tanzania.
“Mwaka huu tumekuwa zaidi na katika kuthibitisha hili Wiki ya maoneshoya mavazi ya Swahili inapeleka maonesho hayo kwa mara ya kwanza kabisa Arusha ambapo ni makao makuau ya umoja wan chi za afrika na baadae onesho lenyewe kufanyika jijini Dar es Salaam, tukiwa na lengo kubwa la kuongeza uelewa wa mavazi, na daima kuwa wa kwanza kutimiza malengo mbalimbali katika tansia nzima ya mavazi,.” Alisema Mustafa Hassanali
Mwaka huu maonesho ya mwanzo yatafanyika katika hoteli ya Mount Meru tarehe 8 Oktoba 2011 kuanzia saa mbili usiku kwa namna ya kipekee kutoka kwa wenyeji wetu Hoteli ya Mount Meru.
“Katika maonesho haya wabunifu zaidi ya 15 kutoka sehemu mbalimbali Tanzania wataonesha mavazi yao vilevile kutakuwa na burudani kali kutoka kwa wasanii wa hapa hapa nyumbani nah ii ni katika kukuza kazi za wabunifu wa Kitanzania na Afrika Mashariki mikoani alimalizia.” Hassanali
.
Katika kutanua wigo wanMaonesho ya wiki ya mavazi ya Swahili imeona njia mbalimbali za kukuza mavazi ya kinyumbani na watu wazungukao tansia hii ya mavazi na kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya maonesho ya mavazi Afrika Mashariki na Kati inazindua rasmi tuzo za maonesho ya wiki ya Swahili katika kuwatambua wadau mablimbali wa tansia hii na wale wanaoizunguka pia.
Katika tuzo hizi wananchi wataruhusiwa pia kufanyaa maamuzi katika tuzo hizi ambapo watapiga kura kupitia vyombo mbalimbali na kura hizo zitahakikiwa na PKF Tanzania na washindi watatunzwa tuzo hizo katika tafrija ya utoaji wa tuzo za wiki ya mavazi ya swahili itakayofanyika tarehe 12 Novemba 2011 na baadhi ya kategori zinazoshindaniwa ni pamoja na Mbunifu bora wa mwaka wa mavazi, Mbunifu bora wa mavazi anayechipukia, Mwanamitindo bora wa mwaka wa kike, na Mwanamitindo bora wa mwaka wa kiume na zinginezo
“Vilevile bila kusahau uwepo wa kizazi kipya nchini Tanzania, kwa mara ya kwanza pia maonesho ya wiki ya Swahili itazindua shindano la utengenezaji na ubunifu wa tisheti huku lengo kuu likiwa kuhusisha vijana na ubunifu wao katika kukuza na kuendeleza familia yetu kimavazi hasa tukizingatia kwa mwaka huu tunasherekea miaka 50 ya Uhuru.” aliongezea Meneja mradi wa Wiki ya maonesho ya mavazi ya Swahili Gillian Rudumamu
“Tunamalengo ya kutangaza biashara ya mitindo katika mataifa mbalili. Ningependa kuwashukuru washirika wetu wote,na wale wote waliotuunga mkono kuanzia miaka ilioyopita na hata sasa.Na pia ningeomba kutoa wito kwa jumuiya na mashirika mbalimbali kutuunga mkono mwaka huu katika maonesho ya mavazi ya wiki ya Swahili.”alisema Afisa habari na mahusiano Enstenium Mgimba
Swahili fashion week 2011 imedhaminiwa na ,the home of Swahili Fashion Week - Southern Sun, EATV, East Africa Radio, Precision Air, BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania), Amarula, Ultimate Security, REDD’S original, Image Masters, Global Outdoor Ltd, Vayle Springs Ltd, Eventlites, Nipashe, Perfect Machinery Ltd, Michuzi blog, PKF Tanzania and 361 Degrees.
0 comments:
Post a Comment