Nafasi Ya Matangazo

October 27, 2011

Afisa mazingira wa Airtel Tanzania Mkama Manyama (kushoto)  akimkabidhi mfano wa hundi ya shilling million tatu kwa Katibu mkuu wa SHIMIWI  Ramadhani Sululu (wapili  kulia) ikiwa ni udhamini wa Airtel kwenye michezo ya SHIMIWI ambayo itafanyika mwaka huu mkoani Tanga. Wakishuhudia makabidhiano hayo ni  Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde (katikati) na Naibu Katibu wa SHIMIWI  Moshi Makuka.

********************************
  • Upandaji miti kufanyika katika  uzinduzi wa michezo ya SHIMIWI
 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Kampuni ya Tanzania Leaf Tobacco Company (TLTC) leo zimetangaza dhamira yao katika kutunza mazingira kwa kuchangia na kushiriki zoezi la kupanda miti mkoani Tanga.

 Tukio hili la kupanda miti litakafanyika mwanzoni mwa mwezi Novemba kama sehemu ya ufunguzi wa  michezo ya SHIMIWI itakayofanyika kitaifa mwaka huu mkoani Tanga.

 Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Afisa Mazingira wa Airtel Tanzania  Bwana Manyama Mkama alisema “Airtel Tanzania kwa kushirikiana na TLTC  tutapanda  miti zaidi ya elfu tatu katika shule ya sekondari ya ufundi  Tanga na shule ya sekondari ya kilimo Galanosi ikiwa ni katika kuendeleza mchakato uliowezesha   miti mengine zaidi ya elfu tatu kupandwa katika maeneo ya barabara ya Sahare, Shule ya Sekondari Kihere, Kombozi, Yusuf Makamba, pamoja na Shule ya Msingi Msamaweni na TLTC mwaka jana.

 Pamoja na kupanda miti Airtel Tanzania tunadhamini mashindano haya na kutoa kiasi cha shilling milion tatu kama ikiwa ni udhamini wetu pia kufanikisha mashindano ya SHIMIWI

 Hii ni moja kati ya jitihada tulizonazo katika kutambua umuhimu wa mazingira na kuyatunza.

 Airtel na TLTC tumejiunga na waandaaji wa mashindano ya SHIMIWI kukamilisha jitihada hizi baada ya  kutathmini mchanganuo wao ulioainisha kupambana na changamoto mbalimbali zinazokumba jamii na nchi kwa ujumla zikiwemo kumomonyoka kwa udongo, kuongezeka kwa  gesi ya ukaa inayopelekea kuongezeka kwa joto kwenye uso wa dunia na nyingine nyingi ambapo hupelekea nchi kuwa na uhaba wa chakula na maji.

 Airtel Tanzania imekua ikichangia sekta mbalimbali ikiwemo elimu kwa kugawa vitabu mashuleni, kuinua michezo nchini, kuboresha mawasiliano hasa vijijini na katika mradi huu, imejikita kutunza mazingira kwa kupanda miti mkoani Tanga. Ni imani yetu kuwa Airtel na TLTC tumechukua hatua sahihi kwa kuhakikisha mazingira yanatunzwa kwa kushirikiana na SHIMIWI mwaka huu kupanda miti mkoani Tanga.

 TLTC ni wadau washiriki katika mipango mbalimbali ya kutunza misitu Tanzania ikishirikiana na wazalishaji wa tumbaku katika mikoa yote. TLTC tumelenga katika kuwaelemisha na kutoa mafunzo kwa wakulima katika kupanda vitalu na kutengeneza mashamba ya miti, kwa vile miti ni sehemu ya uzalishaji wa tobacco TLT inashirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikiksha inaimarisha uzalishaji bora wa bei nafuu na uunguzaji yakinifu. Hadi ifikapo mwaka 2020 TLTC inadhamiria kuwa imefikia kiwango kikubwa cha upandaji wa vitalu vitakavyo wasaidia wakulima wa Tobacco kuacha kutegemea rasilimali ya misitu iliyopo sasa.
Posted by MROKI On Thursday, October 27, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo