Nafasi Ya Matangazo

September 27, 2011

Na Andrew Chale, Bagamoyo
BENDI muziki wa dansi Twanga Pepeta 'wanasugua kisigino' inayotamba Bongo usiku wa kuamkia leo waluifunika kwa shoo kali wakati wa uzinduzi wa tamasha la 30 la sanaa na utamaduni wa chuo cha Bagamoyo.

Katika shoo hiyo ya aina yake, Twanga iliweza kutikisa vilivyo na kuamsha shangwe na vifijo kwa mashabiki hao hasa pale walipopiga nyimbo zao mpya na za zamani ndani ya ukumbi huo wa TaSUBa hali iliyowainua mashabiki kwenda jukwaani kuselebuka.

Miongoni mwa waliotia fola ni pamoja na wanenguaji wote wa bendi hiyo wakiwemo huku Mwumin Mwijuma 'mtoto wa Bagamoyo' aliimba kwa hisia kali akisaidiana na Ruiza Mbutu na wengineo kwa vibao hivyo vipya na vya zamani.

Awali kabla ya Twanga kutumbuiza vikundi mbalimbali vya ngoma na sanaa kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani vilitumbuiza ukumbini hapo huku umati mkubwa ulifurika kushuhudia maonyesho hayo wakiwemo wageni wa ndani na nje.

Tamasha hilo la sanaa la 30 limeanza Juzi na linatarajia kuisha Octoba Mosi mwaka huu na litafungwa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Vijana na Michezo, Emanuel Nchimbi.
Posted by MROKI On Tuesday, September 27, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo