Nafasi Ya Matangazo

August 22, 2011

JAJI mstaafu na mwenyekiti wa Bodi ya Serengeti Breweries  Limited, Mark Bomani amewaasa wanachama wa Sherehe Arts  Association (SAA)  kwa kufanikisha kuanzisha SACCOS  ambayo itasaidia kuendeleza chama na wanachama.

Boban alisema hayo mapema leo  jijini Dar es salaam, kwenye  semina ya kuboresha  Sanaa na Ujasiliamali iliyoandaliwa na SAA,kwenye ukumbi wa City Style Hotel, Sinza, ambapo Jaji Bomani alikuwa mgeni rasmi na kuwataka wanachama wote kufanya kazi kwa umoja na mshikamano ilikuendeleza malengo waliokusudia.

“Nawapongeza kwa jambo hili na hapa mulipofikia ni ishara  ya matunda ya kuendelea zaidi, maana Taifa bila nyie hakuna kingine nawaombeni muendeleze SACCOS kwa njia sahihi na wala I kiujanjaujanja na hapo mutayaona matunda yake zaidi” alisema  Jaji Bomani.
Jaji Bomani pia alikabidhi tuzo kwa wanachama waliofanya vizuri kwa mwaka 2010-2011, sambamba na kukubidhi vitambulisho kwa wanachama wapya watano.

Pi a Jaji Bomani  aliweza kujiunga kuwa mwanachama wa SACCOS hiyo ambapo aliweza kuchangia kiasi cha Milioni moja kama mchango wake ilikuiendeleza na kusisitiza  wanawake wajitokeze kwa wingi kwenye maswala ya  ushehereshaji pamoja na kujiunga na SAA kama mkombozi wao.

Aidha, katika semina hiyo afisa ushirika  wa wilaya ya Kinondoni, James Mvungi aliweza kutoa nasaha za kuboresha SACCOS  hiyo sambamba na kuwathibitishia rasmi juu ya usajili wao huo na Agosti 28 mwaka huu itazinduliwa rasmi.

SAA  kinawaunganisha wasanii mbalimbali wanaokutana kwenye sherehe mbalimbali nchini wakiwemo washehereshaji/walezi (Mastars of Ceremony-MC),Wapiga muziki –DJ, WAPISHI WA VYAKULA VYA SHEREHE, Wapuliza matarumbeta kwenye sherehe na wapiga picha mbalimbali kwenye sherehe
Katika semina hiyo pia zilitolewa mada mbalimbali ikiwemo huduma kwa wateja, iliyotolewa na Mc mkongwe, Mackie Mdachi,Huduma ya vyakula  ilitolewa na Frank Kavembe.
Posted by MROKI On Monday, August 22, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo