Mkoa wa Pwani hususani eneo dogo kutoka Kongowe hadi Mlandizi, Wilayani Kibaha huenda ndo likawa linaongoza kwa kuwa na vituo vingi vya kuuza mafuta hapa nchini. Camera ya Father Kidevu iliyokuwa safari kutoka Dar es Salaam kuelelkea Arusha ilifanikiwa kuvinasa baadhi tu ya vituo hivyo na vibavyotaraji kujengwa. Safiri nami uvione na hivi ni baadhi tu ya vituo vya upande wa kushoto tu ukitoka Dar kwenda Chalinze.
Wengine baada ya wenzao kujenga wao wakaamua kubuni aina mpya ya paa la vituo vyao.
Vipya bado vinajengwa ...
...na viwanja vinazidi kusawazishwa kwa ujenzi zaidi wa vituo vipya.
Utitiri huu wa vituo vya mafuta huenda ukawafanya wengine wakose majina na sasa kusema hivi ...ili dereva aingie anakotaka.
Akia Muro nao siku hizi kama warabu nao wanavituo vya mafuta kwa majina yao.




0 comments:
Post a Comment