Nafasi Ya Matangazo

July 15, 2011

Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa tenki la maji lenye uwezo wa  kuhifadhi ujazo wa lita za maji 50,000 lililojengwa na TBL kwa msaada wa sh. milioni 15 katika Kijiji cha ya Lugarawa, wilayani Ludewa, Iringa.Anayeshuhudia uzinduzi huo uliofanyika hivi karibuni sambamba na kukabidhi mradi huo, ni Mbunge wa Viti Maalum Pindi Chana (CCM).
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Pindi Chana (CCM),wa pili kushoto, Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (wa tatu kushoto), Afisa Tawala wa wa Wilaya ya Ludewa,Charles Keiya na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Lugarawa, Mathias Kihaule (kushoto) wakifurahia wakati TBL ilipokabidhi tenki la maji lenye ujazo wa lita 50,000 za maji katika Kijiji cha Lugarawa, wilayani Ludewa hivi karibuni.Ujenzi wa tenki hilo  umegharimu sh.milioni 15 zilizotolewa na TBL.
Kwaya ya Umoja wa Wanawake wa CCM, wa Kata ya Lugarawa  wakitumbuiza katika hafla ya makabidhiano hayo.
Posted by MROKI On Friday, July 15, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo