Mbunifu wa Mitindo, Mtanzania Mustafa Hassananli (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William Lukuvi wakati wa siku ya kwanza ya maonesho ya HARUSI TRADE FAIR 2011 yanayoendelea katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam .
Mkurugenzi wa MH Galary Moiz Hussein akiwakilisha katika maonesho hayo makubwa ya Harusi, ambapo masuala ya Picha ni muhumu katika kuweka kumbukumbu. MD Digital Company inapokea mchango kubwa sana kutoka MH Galary.
Mkurugenzi wa MH Galary Moiz Hussein akiwakilisha katika maonesho hayo makubwa ya Harusi, ambapo masuala ya Picha ni muhumu katika kuweka kumbukumbu. MD Digital Company inapokea mchango kubwa sana kutoka MH Galary.
Malaika Event Rentals Booth at Diamond Jubilee
Mmoja wa waliotembelea maonyesho ya HARUSI kwenye ukumbi wa DIAMOND JUBILEE wakisiliza maelezo toka kwa washiriki wa maonyesho hayo.
Kumbu kumbu ni muhimu katika Harusi, Send, na tafrija zozote ambazo hapo baadae ungependa kuopna sherehe yako ilifanyikaje. Makampuni ya picha kama MD Digital Company, MH Galary na GRM Production, ndio jibu la swali la nani atafanya kazi hii.
Wfanyakazi wa Blue Pearl Hotel & Apartment wakijiweka sawa kwa maonyesho ya HARUSI ndani ya Diamond.
Maonyesho ya Harusi yaliosubiriwa kwa hamu na wadau mbalimbali wa masuala ya harusi na watarajiwa wa harusi yameanza leo katika ukumbi wa DIAMOND JUBILEE huku yakiwa na washiriki zaidi ya 51 waliochukua mabanda kwa kuonyesha na kuuza biashara zao.
Wakizungumza kkwa nyakati tofauti tofauti washiriki hao ambao wamejitokeza kwa wingi, waliyasifu maonyesho ya mwaka huu na kusema kuwa yamekuwa hai na mvuto wa aina yake, kwa kuwa mambo mengi yameongezeka kwa mwaka huu.
"Tulishiriki mwaka jana, na mwaka huu pia, ila mwaka huu yamekuwa mazuri zaidi na yenye kupangiliwa zaidi, kwa kweli waandaaji wamejipanga vilivyo" alisema mmoja wa washiriki toka kampuni ya picha ya GRM.
Maonyesho ya mwaka huu yameongezewa ladha kwa kuongezewa vitu mbaliombali, ambapo mbali na kuongezeka kwa nafasi na mabanda, pia kuna upya wa vitu kama 'mdahalo wa Harusi' ambapo wataalamu waliobobea katika masuala ya harusi watazungumza na wale watakaotembelea maonyesho hayo.
Huku jarida la kwanza na la aina yake la kitanzania 'HARUSI MAGAZINE' chini ya usimamizi wa mbunifu wa mavazi maarufu nchini Mustafa Hassanali likisambazwa ukumbini hapo kwa toleo lake la kwanza.
Wadau wote na wakaazi wa jiji la Dar ess salaam wanakaribishwa sana katika maonyesho haya ya siku tatu yanayoendelea ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee.
0 comments:
Post a Comment