Nafasi Ya Matangazo

April 06, 2011

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda(kushoto) akisalimiana na mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Clement Mshana mara baada ya kuzungumza na maafisa habari, Elimu na Mawasiliano wa Wizara, Idara, Taasisi za serikali, Mikoa na wakala leo mjini Dodoma.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Clement Mshana nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
 Spikawa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda(wa nne kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na maafisa Habari,Elimu na Mawasiliano wa Wizara, Idara, Taasisi za Serikali na wakala wa serikali nje ya Ukumbi wa Pius Msekwa mara baada ya kuzungumza nao.Viongozi wengine ni Naibu waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenela Mkangara (wa tatu kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Clement Mshana(wa tano kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Habari,Uhusiano na Elimu kwa Umma Bungeni Bw. Jossey Mwakasyuka(wa pili kutoka kushoto).
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Mh. Jenista Muhagama(katikati) akiongea na maafisa Habari,Elimu na Mawasiliano wa Wizara, Idara, Taasisi za Serikali na wakala wa serikali ndani ya Ukumbi wa Pius Msekwa leo mjini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi na Mkurugenzi wa Idara ya Habari,Uhusiano na Elimu kwa Umma Bungeni Bw. Jossey Mwakasyuka (kulia).
Posted by MROKI On Wednesday, April 06, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo