Nafasi Ya Matangazo

March 10, 2011

Marehemu John Luanda (kwenye kiti) akiwa na familia yake wakati wa uhai wake akipatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Beda Msimbe "Lukwangule"  mama na wadogo zangu pamoja na kaka binadamu lubuko katika picha ambayo Luanda mwenyewe akiwa hospitalini aliomba apige na familia yake..

Na Mwandishi wetu



Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania John Luwanda amefariki dunia Muhimbili leo mchana baada ya kuugua kwa siku kadhaa.

Kwa mujibu wa mtoto wake Beda Msimbe, mtangazaji huyo wa zamani ambaye alistaafu kazi hiyo mwanzoni mwa miaka ya 1990 alikuwa amelazwa hospitali ya Muhimbili akisumbuliwa na kisukari huku akifanyiwa uchunguzi wa kansa ya kibofu cha mkojo.

Mtoto wake huyo alisema kwamba madaktari walimwambia kwamba baba yake alikufa kutokana na ugonjwa wa uti wa mgongo.

Luwanda ambaye atakumbukwa zaidi na watu wa vikundi vya sanaa kwa uandalizi wa michezo ya kuigiza ya radio,mara baada ya kustaafu alikuwa anaishi katika kijiji cha Goba akilima bustani na kufuga.

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake Goba kijijini na anatarajiwa kuzikwa Jumamosi wiki hii.

Luwanda ameacha mke watoto 6 na wajukuu 20.

Posted by MROKI On Thursday, March 10, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo