Nafasi Ya Matangazo

August 09, 2010

WASHIRIKI 31 wa fainali za Vodacom Miss Tanzania 2010 wanataraji kuingia kambini katika Hoteli ya Giraffe iliyopo Jangwani Beach, Jumatatu ya Agosti 16 2010.

Taarifa kutoka kwa waandaji wa Shindandi hilo, Kampuni ya Lino International Agency inasema kuwa warembo hao wanatakiwa kuripoti katika ofisi za Kampuni hiyo zilizopo katika makutano ya mtaa wa Samora na Mkwepu saa 3.00 asubuhi kabla ya safari ya kuelekea Kambini kuanza.

Aidha taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Lino International Agency , ambaye pia ni Mratibu wa shindano la Vodacom Miss Tanzania Hashim Lundenga imesema washiriki wote wanatakiwa kufika katika sik,u na saa iliyopangwa na si vinginevyo na yeyote atakaye chelewa kufika bila sababu maalum na bila kutoa taarifa atakuwa amejitoa katika fainali hizo za mwaka huu.

Walimbwende wanaotakiwa kuingia kambini majina yao na Kanda wanazotokea katika mabano ni:-

Ester Dennis na Gloria Kaale (CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM).
Shadia Mohammed, Furaha David na Mary Kagali (NYANDA ZA JUU KUSINI).
Bahati Chando, Salma Mwakalukwa na Consolata Lukosi (KANDA YA ILALA
Beatrice Premsingh, Willemi Etami na Pili Issa (KANDA YA KATI),
Flora Florence, Mary Adam na Angelina Ndege (KANDA YA MASHARIKI),
Alice Lushiku, Irene Hezron na Amisuu Malick (KANDA YA KINONDONI)
Genevive Emmanuel, Anna Daudi na Britney Urassa (KANDA YA TEMEKE),
Glory Mwanga, Prisca Mkonyi na Jally Murei (KANDA YA KASKAZINI).
Gloria Mosha na Christine Justine (KANDA YA CHUO KIKUU HURIA),
Flora Martin, RachelSindbad na PendoSam (KANDA YA ELIMU YA JUU),
Fatma Ibrahim, Buduri Ibrahim na Margareth Godson (KANDA YA ZIWA).

Fainali za mashindano hayo makubwa ya Urembo nchini yanataraji kufanyika Septemba 11 2010 jijini Dar es Salaam
Posted by MROKI On Monday, August 09, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo