Nafasi Ya Matangazo

June 25, 2010

Kambi ya Makapera ya Benki ya Akiba Commercial Bank Makao Makuu jijini Dar es Salaam imevamia na kijana mmoja na kupora mmoja wa watendaji wake wakuu, Bi. Fadhila Charles (pichani kushoto). Kulia ni Msimamizi wake Neema Kakoko kutoka Don Consult LTD. Sara Sakaya kutoka Dimond Trust Bank akimimina mvinyo katika glass tayari kwa kutakiana heri.Muda muafaka wa kutakiana heri huko Fadhila aendako. Kulia ni Neema. Wazazi nao waligonganisha glass zao kumtakia safari njema binti yao.
Pia FadhilaBi Harusi mtarajiwa alikata keki ambayo iliashiria kuwakaribisha wageni wote katika chakula cha usiku kilicho andaliwa kwaajili yao.
Aliwakabidhi wafanyakazi wenzake wa ACB moja ya keki hizo.
ACB Famili ilifurahi sana kwa zawadi hiyo.
Hiki ni chakula kikuu cha Wapare kinaitwa Kishumba na hutengenezwa kwa Maharage na ndizi na wakati mwingine hutengenezwa kwa Viazi vitamu na maharage lakini hukiita Kishumba. Ni kitamu sana usisikie.
Fadhila alimkaribisha mumewe mtarajiwa chakula hicho tofauti na wengine, alikata Kishumba na baadae kumlisha Mumewe Mtarajiwa.
Baadhi ya waalikwa wakiwa ukumbini.
Fadhila akiwa na wazazi wake Bawana na Bibi Bendera.
Familia ya ACB katika picha ya pamoja na mfanyakazi mwenzao walipohudhuria sherehe ya kumuaga kabla ya kufunga ndoa.
Huyu ndiye Kamanda aliyevunja ngome ya ACB na kupora huyu kimwana. Mungu awabariki.
Picha zote na MD Digital Company -075 5373 999/071 7002 303

Posted by MROKI On Friday, June 25, 2010 1 comment

1 comment:

  1. We Mroki we!

    Hao wageni waalikwa laiti wangejua wanavyoniboaga mimi na hiyo tabia yao na fasheni yao ya kutuonyesha hayo MANYONYO yao sisi yanayokuwa kama MAPUTO! Khaa!

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo