Nafasi Ya Matangazo

April 07, 2010

Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume(katikati) Rais Jakaya Kikwete,pamoja na vingozi wengine wa Kitaifa na wananchi wakiwa katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,Rais wa Kwanza wa Zanzibar,wakimuombea dua katika kumuenzi tokea kufa kwake na kutimia miaka 38, katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar jana.Kutoka kushoto ni Rais wa Zanzibar , Amani Abeid Karume, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji,Makamu wa Rais Dk Ali Mohammed Shein na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha wakisoma Khitma ya kumuombea Dua Marehemu Abeid Karume, iliyofanyika jana ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.Baadhi ya wananchi wakisoma khitma ya kumuombea dua marehemu Mzee Abeid Karume,muasisi wa ASP na Rais wa Kwanza wa Zanzibar,kwa kutimiza miaka 38 tokea kifo chake katika ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui leo.Mjane wa Muasisi wa mapinduzi ya Zanzibar, Mama Fatma Karume pamoja na mke wa Rais wa Zanzibar Mama Shadya Karume wakishiriki dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyosomwa wakati wa kilele cha maandamano ya UVCCM kumuenzi muasisi huyo juzi mjini Zanzibar.Wake za viongozi mbalimbali pamoja na viongozi wengine walijumika pamoja kumuombea dua Marehemu Mzee Karume katika kaburi lake lililopo Ofisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar jana.
Posted by MROKI On Wednesday, April 07, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo