JESHI LA POLISI NA KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI TIGO WAUNDA KIKOSI KAZI KUDHIBITI WIZI WA MIUNDO MBINU
Jeshi la polisi Kamanda Dar es salaam kwa kushirikiana na kampuni ya simu za mkononi Tigo wameunda kikosi kazi (Task force) kwa madhumuni ya kudhibiti wizi wa miundo mbinu kama vile betri za minara ya simu, vipuri vya majenereta na mafuta.
Akiongea na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi kanda maalum ya polisi Dar es Salaam Kamanda S. H Kova alisema Wizi huo wa miundo mbunu umekuwa ukitokea mara kwa mara katika jiji la Dar es salaam na mikoani na sasa umekithiri. wezi hao wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali za wizi kwa kujifanya wao ni watumishi wa kampuni hiyo na hatimaye kufanikiwa kuiba.
Wizi huo umegharimu mamilioni ya fedha dhidi ya kampuni ya Tigo. hivyo kuathiri mapato ya kampuni ya Tigo na nchi yetu. Tigo kwa kushirikiana na jeshi la polisi kanda maaalum limeanzisha kikosi kazi kitakachokuwa na kazi ya kufanya msako na tayari kikosi kazi hicho kimefanikiwa kukamata betri 48 na watuhumiwa wawili wamekamatwa majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi Ili kupata ufanisi wa operesheni hiyo wananchi wameombwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kwa namba 0715 123888, mtu yeyote atakayekuwa na taarifa atume ujumbe, ujumbe utakuwa ni bure hautakuwa na tozo yeyote.
Aidha kampuni ya ulinnzi ya Kiwango inayoshughulikia ulinzi wa minara itakuwa inatumia namba 0715 123444 kwa kupitia namba hizo utoaji taarifa utakaombatana na mafanikio utamfanya mtoaji taarifa kufanikiwa kupata donge nono lisilopungua shilingi milioni moja na kuendelea hii ni kwa kutokana na uzito wa taarifa yenyewe.
Pia wananchi wameonywa kutonunua betri za aina hiyo kwa matumizi yasiyo kusudiwa kwani kitendo cha kununua betri hizo kitakuwa ni kinyume cha sheria na hivyo kushitakiwa mahakamani
0 comments:
Post a Comment