Nafasi Ya Matangazo

November 06, 2009

Mwanadada mahiri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya kutoka kundi machachari jijini Dar es Salaam la Nyumba ya Vipaji (THT) Doureen au maarufu Pipi siku si nyingi anataraji kupakua nyimbo moja mpya kati ya kadhaa zitakazo unda albam yake mpya.

Pipi anapasha yakuwa uamuzi wa wimbo gani utoke kwanza kati ya hizo alizo nazo bado unampa utata.

"Niko njiapanda ku decide nitoe Nilikupenda au Ukiniacha au Unapokuwa mbali...." anasema Pipi.

Anasema kuwa Nyimbo hizo amezifanya katika studio tofauti tofauti ili kupata vionjo na ladha tofauti kutoka kwa maproduza walio bobea katika fani hii.

"Nimefanya kazi katika stuo tofauti kama Sound Crafters,Bongo Records,Jazz Records na Studio 69 zote za hapa nchini"

Maudhui katika nyimbo hizo ni maisha na mapenzi ambayo daima hayajitengi katika shughuli za kila siku za mwanadamu yeyote yule duniani.

"maudhui ni kwa jamii nzima ina combination ya mapenzi na maisha...album will be out soon..."
Posted by MROKI On Friday, November 06, 2009 1 comment

1 comment:

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo