Nafasi Ya Matangazo

November 05, 2009

Waswahili wamesema “mficha maradhi kifo humuumbua” sasa imefika muda wa kuutoa ukweli halisi ili tuweze kujua ni vipi haswa tunaweza kujikomboa na matatizo yaliyotufika.

Inaeleweka kuwa watanzania sote tupo Mysore au sehemu nyengine ya India kwa masomo, sidhani kama kuna mzee yoyote atakae ruhusu mtoto wake kuja India kutenda lolote baya pasi na kusoma.

Tunaelewa ya kwamba tuna matatizo sisi wenyewe watanzania ila sio kikwazo cha kutopata haki yetu, matatizo tuliyonayo sisi ni kupreserve culture yetu, hivi labda niulize, kwa mtu niliyeishi Tanzania kwa miaka zaidi ya 20 na kupractice our culture kwa miaka yote hayo nitaweza kuiacha pembeni kwa ghafla moja? I mean so sudden? Hii ni kitu kisichowezekana hata kidogo.

Naomba turudi kwenye vitabu vinasemaje juu ya “multiculturalism” je India haithamini au kulinda haki na tamaduni za minority? Je tuangalie Article 29 and Article 30 ya katiba ya India inasemaje? Kwa vipengele hivyo mtakubaliana nami kuwa India italinda haki na tamaduni zetu based on minority as far as we are here legally.Itakuwa unafiki kama nitasema wanafunzi wa mysore tupo safi hatuna kosa lolote, tunafanya makosa mbalimbali, kweli tunakunywa pombe, tunafanya parties etc. Ila kwa muda wote niliokaa Mysore sijawahi kuona au kusikia mtanzania ameiba, amebaka, ameua au amefanya kosa lolote lile ambalo ni jinai au linalohitaji state of mind.

Though ni vigumu kuweza kubadilisha attitude ya wahindi kwetu ila naimani kuna jambo linaweza kufanyika likatusaidia watanzania tuliowengi hapa Mysore.

Wanafunzi wenzetu kutoka nchi mbalimbali tumeshuhudia wakipata matatizo kidogo tu basi maafisa wa ubalozi wa nchi zao wamefika kutatua diplomatically hata kama hiyo kesi ni kubwa vipi.

Hebu tuangalie mfano wa wale wazungu waliomuuwa mtanzania pale dar ilikuwaje hadi wakaachiwa just because kuliendeshwa mazungumzo diplomatically kutatua tatizo lile, ndivyo inavyotokea kwa nchi nyengine hapa mysore.

Hali imekuwa si hivyo kwa watanzania wa India hususan watanzania tunaoishi Mysore.Sitakosea nikisema kuwa ubalozi wetu hauna msaada hata kidogo kwetu kuanzia miaka hiyo ya nyuma hadi muda huu, tulibahatika kukutana na maafisa wa ubalozi mara mbili katika miaka karibia 6 sasa na hapo ilikuwa na sababu maalum ni kwakuwa kulikuwa na watoto wa makamu wa rais wa Tanzania na walikuja on their request sio kwa sababu ya watanzania.


Kuthibitisha kauli yangu nitatoa mifano hai michache ambayo italinda kauli hii;-

1. Mwaka 2006, watanzania walipigwa hadi kutaka kufa huku polisi wakiangalia bila ya msaada kwa watanzania na hatimae wakawafungulia kesi hao waliopigwa, uongozi ukawasiliana na ubalozi kwa kuomba msaada hata wa maarifa, ila jawabu likawa “ sasa sisi tufanye nini nyinyi wakorofi” hilo ndilo jawabu la ubalozi tunaotegemea kama mzazi wetu tukiwa nje ya nchi yetu2. Mwaka 2007, watanzania wa Bangalore walikuja Mysore kujuana na watanzania wenzao na tukawakaribisha kwa michezo mbalaliazania wenzao na tukaandaliatukiwa nje ya nchi yetu

2., uongozi ukawasiliana na ubalozi kwa kuomba imbali ikiwemo mpira wa miguu na wa mikono, mwisho tuliomba ruhusa kufanya party katika ukumbi mmoja maeneo ya mjini na tulikubaliwa, mwisho wa yote askari walikuja na kuwatowa watu wote ndani ka kuanza kuwapiga bila ya hatia ati kwasababu wanayoiita nuisance, ambapo kibali walitoa hao wenyewe. Uongozi uliwasiliana na ubalozi na jawabu likawa “ kwani mlienda kufanya nini huko sisi hatuna msaada wa kuwapa”

3. Mwenzi mmoja nyuma mtanzania amepata ajali na kumgonga mpita njia, hatimae mwenda kwa miguu huyo alifariki hapohapo, na mtanzania huyo aliwekwa ndani kwa kosa la kuuwa, uongozi uliwasiliana na ubalozi kwa msaada, ila jawabu likawa “kwani alikuwa anafanya nini barabarani muda huo?” na kweli hawakutoa msaada wowote.

4. Kesi ya sasa ambayo iliyopelekea kila kona wa watanzania kuelewa kilichopo Mysore, watanzania walikamatwa nyumbani kwao kwa makosa ambayo hata aliekuwa hasomi sheria atajua ni uonevu, hivi nini maana ya Unlawfull assembly? Ni pale watu zaidi ya watano wakikusanyika pamoja na kuwa na nia mbaya kisheria, je hawa watanzania kweli wamecommitt unlawful assembly? Lakini hata hivyo uongozi ulivyowasiliana na ubalozi kupata msaada ili wenzetu wapate dhamana jawabu likawa “sisi hatuna umeme hivyo hatuwezi kufanya lolote, wewe tutumie copy za magaazeti” je wewe kama mzazi unaetegemewa unaweza kusema hayo unaposikia mtoto wako yupo ndani?

Hayo ni baadhi tu ya mambo yanayotokea Mysore na majawabu tunayopata kutoka ubalozini kwetu, cha ajabu ni pale wanaposema uongo ya kuwa wana msaada kwetu, juzi walitangaza wanashughulikia dhamana ya waliwekwa ndani wakati kumbe tayari sisi wenyewe tulishachangishana na kuweza kupata dhamana hiyo. Balozi wetu KIJAZI alitafuta namba ya advocate baada ya bail kupatikana tena kutokana na kuona mambo yamekuwa makubwa.

Swali letu je
hivi ubalozi wetu ni lini utakuwa na msaada kwetu au hadi wasikie tumekufa?

Je muheshimiwa Rais Kikwete unajua kinachotupata watanzania tuliopo India?Sasa tunatamka wazi watanzania wa Mysore tumechoka tena tumechoka na majibu mabaya tunayopata kutoka ubalozini kwetu, sasa tunaamua kutafuta haki yetu sisi wenyewe, Tunamuomba Mwenyezi Mungu atulinde na mchakato huu.

Hivi huyu mzee anaeitwa MWAMANENGE yupo ubalozini kwa manufaa ya nani? Ikiwa sisi tunaehitaji msaada wake anajibu yeye hana msaada wowote kwetu, mfano mdogo alipokuja Makamo wa Rais hapo Bangalore, watanzania wa Mysore waliomba msaada wa kukodishwa basi la kufika Bangalore kumuona Makamo wetu ila jawabu lilikuwa huu mkutano hauwahusu ni wa watu wa Bangalore je huyu ni kiongozi anaefaa kwetu?Watanzania wa Mysore tumeamua kushikamana na tunatafuta haki yetu kwa kutumia njia mbadala zaidi ya ubalozi uliwekwa kwa manufaa ya watu wachache.

Hii inaitwa ACTION VITENDO.MUNGU IBARIKI TANZANIAMUNGU TUBARIKI WANAFUNZI WA TANZANIA
Posted by MROKI On Thursday, November 05, 2009 4 comments

4 comments:

  1. Poleni sana watanzania wenzetu,inasikitisha sana kama hali ndio hiyo,sasa huo ubarozi wa Tanzania huko unafanya kazi gani zaidi? hizo ndio moja ya sababu ya kufungua ofisi za ubarozi huko kama hawana msaada basi bora zifungwe!labda kwa ushauri wewe ulietoa hii mada hapa,siku hizi si watu wanaweza kuwasiliana moja kwa moja na rais? ni bora mkafanya hivyo,pia hii mada ungemtumia pia na Issa Michuzi,yeye blog yake pia inasomwa na watu wengi sana hata hao wakubwa serikalini,hili sio la kufumbia macho linastahili kujadiliwa kwa kina na ushauri zaidi.

    Poleni sana jamani,kweli Tanzani viongozi wake ni bongo lala kila kona yamejaa mafisadi huo ni ufisadi tosha.

    ReplyDelete
  2. MANENO UNAYOYASEMA TUMEFAHAMU NA NYIE MNASEMA KUWA WANAFUNZI NA WAJIBU WENU NI KUFAHAMU NA KUYAELEWA SHERIA INAVOSEMA . IKIWA SHERIA INASEMA HAMRUHUSIWI KUKUSANYIKA . BASI FATENI KWA KUWA NYIE NDIO WAHITAJI.
    2- UKWELI UFAHAMU NCHI TAJIRI PEKEE NDIO INALINDA RAIA WAKE. SIJAONA WALA KUSIKIA NCHI MASKINI IKISUMBUKA AU KUFUATIA RAIA WAKE NJE YA NCHI NA WAKATI MGUMU KWA WANAOISHI NDANI YA NCHI.

    ReplyDelete
  3. Mwamnenge kumbe bado yupo hindustani? mimi nilidhani alirudi nyumbani tangu enzi hizo za kwetu mwaka 47. Balozi nyingi au Watanzania kwa ujumla uzalendo unakuja pale kwenye UCCM tu ndio ninapo shangaa mimi. Wamarekani awe amekosa au hajakosa nje ya nchi yao watamsaidia halafu kama ni kumshughulikia watahaminika naye kwao lakini si kwa watu. It is high time sasa watu wabadilike na kuwa na uzalendo wa kweli ni changamoto kwa balozi zote za Tanzania duniani kuwa kwa ajili ya Watanzania kwanza na sisi tujivunie utanzania wetu sio kutokuwa na tofauti ukiritimba wa nyumbani hadi ugenini.
    Enzi zetu sisi watanzania walipigwa, waliuawawa lakini ndio hivyo Wahindi ni wakatili sana lakini wao sharuh khan alivyowekwa airport masaa matatu Marekani ubalozi wao ulikuja juu ni wakati wa kutunzana ama sivyo uzalendo hauna maana yoyote

    ReplyDelete
  4. poleni sana wadogo zangu , lakini kama mlikuwa hamjui kuwa barozi za tanzania nchi yoyote hazina faida na mtanzania yoyote ... hizo ofisi za barozi ni kwa ajili ya umbea nani kafanya hili na nani kafanya kile ! amini usiamini ubarozi wa tanzania umejaa majungu tu , hebu jamani angalieni wenzetu mfano wa west afrika wanaushirikiano sana ... sisi ni roho mbaya sana sasa kama watoto wanapata matatizo huko india kwenye nchi ya ugenini wakimbilie wapi kama sio ubarozini ? ng´ombe akijeruhiwa malishoni ukimbilia zizini kupata msaada ..au sababu hapo katika tukio hakuna mtoto wa barozi au mkubwa wa nchi ? poleni sana wadogo zangu sana !!!lakini ndio mjifunze mnapowaona wahindi bongo sio wa kucheka nao ni nuksi , mkifika bongo mwendo kupiga mbwa wa kidosi tu , shenzi type hao .

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo