Nafasi Ya Matangazo

October 29, 2009

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi usafiri aina ya Bajaji kwa mwanamkw mlemavu Sara Mageni Sanga aliyekaa chini katika kijiji cha Lupalilo,Wilayani Makete,mkoa wa Iringa jana jioni.Pembeni ya Rais kulia ni mkuu wa mkoa wa Iringa Bwana Mohamed Abdulaziz.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Mlemavu Sara Mageni Sanga hati na vibali mbalimbali vya usafiri aina ya Bajaji mabyo Rais alimkabidhi mlemavu huyo katika kijiji cha Lupalilo,wilayani Makete,Mkoani Iringa jana jioni.Rais Kikwete alifanya uamuzi huo baada ya kuona adha anayopata mlemavu huyo kupitia kipindi kilichorushwa na Televissheni ya taifa TBC One hivi karibuni.Rais Kikwete yupo mkoani Iringa kwa ziara maalumu ya kukagua mashamba ya mifugo.
Mtaalamu wa usindikaji maziwa katika kiwanda cha Kusikindika maziwa mjini Njombe Bwana Geofrey Nyigu(kushoto) akitoa maelezo kwa Rais Jakaya Mrisho kikwete ya mchakato wa kusindika maziwa unavyofanyika katika kiwanda cha kusindika maziwa mjini Njombe, mkoani Iringa leo mchana.Katikati anayeangalia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mohamed Abdulaziz.

Mmiliki wa shamba la mifugo lililopo eneo la Ifunda,Mkoa wa Iringa Bwana Mark Taylor akimwonesha Rais Jakaya Kikwete baadhi ya kondoo wa mfano wanaozalishwa katika shamba hili leo asubuhi.
Bwana Mark Taylor akimwonesha Rais Jakaya Mrisho Kikwete baadhi ya ng’ombe wanaofugwa kwa kuzingatia kanuni za ufugaji bora wakati Rais Kikwete alipotembelea shamba hilo la mifugo eneo la Ifunda wilaya ya Iringa vijijini leo asubuhi.
Posted by MROKI On Thursday, October 29, 2009 1 comment

1 comment:

  1. ivi kwa nini uyo mweupe apo asiwe mweusi..yaani mambo mengine kero tupu..watanzania wafugaji wanafaidika vp na huo mradi,yaani rais apo kafuka

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo