Nafasi Ya Matangazo

September 05, 2009

Watu 25 wamejeruhiwa vibaya na mmoja kufariki wakiwa wanaiba mafuta baada ya lori la mafuta kupinduka na kulipuka leo asubuhi katikaeneo la Mdaula, mkoani Pwani.


Taarifa za Kipolisi toka kwa RPC wa Pwani Absalom Mwakyoma anasema mtu huyo aliyekufa hajafahamika jina lakinianakadiriwa kuwa ni kijana.

Kamanda Mwakyoma, amesema majeruhi 19 wamepelekwa katika Hospitaliya Muhimbili, wawili Tumbi na wanne katika Hospitali ya Morogoro.


Mwakyoma alisema ajali hiyo ilitokea baada ya lori lenye namba zausajili T 102 AFY aina ya Scania, lenye tela namba T270 AUT likiendeshwa na dereva Jorum Krofasi (35) na utingo Masunga Masanja(25) lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza.

Baadhi ya majeruhi waliotambulika ni Juma Mohammed (26), Hamisi Malugwisha (25),Kadili Kiwembe (22), RamadhaniIssa (27), Malik Tingisha (24) na FadhiliMaumba (29).


Watu hao inaaminika kuwa waliojeruhiwawalikuwa katika harakati za kuchota mafuta kwani yalikutwa na madumu na baiskeli nyingi zikiwa zimeegeshwa pembeni mwa eneo la tukio.
Posted by MROKI On Saturday, September 05, 2009 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo