MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA UTALII TANZANIA (TTB) BWANA PETER MWENGUO AKIANGALIA TEMBO WAKATI WA ZIARA YAKE YA KIKAZI KUTEMBELEA SINGITA GRUMETI RESERVES ILIYOKO KATIKA MBUGA ZA SERENGETI AMBAPO ALITEMBELEA LOJI ZOTE TATU AMBAZO NI SASAKWA, FARUFARU NA SABORA YOTE YAPO KATIKA WILAYA YA SERENGETI MKOANI MARA.
MWENGUO AKIFANYA MAZOEZI YA BASKELI WAKATI ALIPOTEMBELEA CHUMBA CHA MAZOEZI CHA HOTELI YA KIFAHARI YA SINGITA GRUMETI RESERVES ILIYOKO SERENGETI MKOANI MARA MWISHONI MWA WIKI.
MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA UTALII NCHINI BWANA PETER J. MWENGUO AKITOA MAELEZO KWA WAANDISHI WA HABARI KWA NINI BAADHI YA MVINYO NA SHAMPENI HUUZWA KWA BEI MBAYA ALIPOTEMBELEA HOTELI ZA KIFAHARI ZA SINGITA GRUMETI RESERVES WILAYANI SERENGETI MWISHONI MWA WIKI. CHUPA ALIYOSHIKA NI YA MVINYO AINA YA PETRUVS AMBAO UNAUZWA KWA DOLA 1,850 KATIKA HOTELI HIYO AMBAO UMEELEZEWA UNAPENDWA SANA NA WATEJA WANATEMBELEA HOTELI HIYO. WAANDISHI WANAOMSIKILIZA NI KHADIJA KHALILI WA TANZANIA DAIMA NA JACOB MGINI WA DAILY NEWS.
WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI KUTOKA WILAYA ZA SERENGETI NA BUNDA MKOANI MARA WAKIWA KATIKA DARASA MAALUM LINALOFUNDISHA MASUALA MBALIMBALI YA UHIFADHI KATIKA LOJI ZA KIFAHARI ZA SINGITA GRUMETI RESERVES WILAYANI SERENGETI. WAMILIKI WA SHULE HIYO PIA WANAENDESHA HOTELI ZA KIFAHARI KATIKA MBUGA HIZO ZILIZOJAA WANYAMA PORI WA KILA AINA.
Hili darasa mbona halionyeshi ufahari wa hoteli zao za kifahari, linawaangusha walibadirishe angalu lionyeshe taswira ya hotel yao, viti, meza, mbao nk
ReplyDeleteFK,
ReplyDeleteNini hatima ya mtanzania wa kawaida katika mali-asili za Bongo??
Kuna punguzo lolote kwa wabongo kutembelea Mbuga zetu? hayo mambo ambayo wahandishi wanatakiwa kuuliza huyu Mkuru-Genzi.