Nafasi Ya Matangazo

February 19, 2009

HOFU imetanda jijini Dar es Salaam kufuatia kutokuwepo kwa Mtuhumiwa Amatusi Liyumba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam ikiwa ni siku chache tu baada ya kupewa dhamana 'tata' iliyotolewa ufafanuzi na mawakili wake Februari 18, 2009.
Liyumba anayetuhumiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka,Benki Kuu ya Tanzania (BoT), leo (Februari 19, 2009 iliamriwa na Mahakama kukamatwa pamoja na wadhamini wake.

Hata hivyo, amri hiyo jana ilionekana kugonga mwamba, baada ya mtuhumiwa huyo kusakwa na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) bila mafanikio.

Alitakiwa apandishwe kizimbani jana, lakini badala yake maofisa wa Takukuru waliambulia kuwakamata wadhamini na wakakiri mahakamani hapo kuwa Liyumba haonekani.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu juzi ilitoa hati ya kukamatwa kwa Liyumba ikiwa ni siku moja tu, baada ya kupewa dhamana na mahakama hiyo katika mazingira ambayo hayakuuridhisha upande wa mashitaka.Hakimu Hadija Msongo alikiri kuwa mahakama hiyo ilitoa hati ya kukamatwa kwa mshitakiwa huyo na wadhamini wake. Lakini hakueleza sababu ya mahakama kutoa hati hiyo, kwa kile alichodai kuwa jalada la kesi hiyo tayari limepelekwa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Liyumba alipewa dhamana baada ya kuwasilisha mahakamani hapo hati ya mali yenye thamani ya Sh milioni 882 wakati alitakiwa kuwasilisha fedha taslimu Sh bilioni 55 au hati za mali zenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

News kamili www.habarileo.co.tz
Posted by MROKI On Thursday, February 19, 2009 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo