
Mwimbaji na kiongozi wa Bendi ya FM Academia Nyoshi El Saadat, Rais wa Wanamuziki Vijana nusura atoe machozi kwa waandishi wahabari leo kufuatia kitendo cha bendi ya Akudo kutaka kumchukua Repawao maarufu Kalijo Kitokalolo a.k.a KUKU (kulia) ambaye amisimamishwa kutokana na makosa ya kinidhamu. Mapema wiki hii Kitokalolo aliripotiwa kupanda katika jukwaa la Akudo na uongozi wa bendi hiyo kumtambulisha kwa mashabiki.

Picha hizi zikimuonyesha Nyoshi akiwa katika sura ya hasira na kuchukizwa na tabia ya kulubuni wanamuziki.

Nyoshi pia aliyesema yeye amesoma mubaya (amesoma sana) mambo ya biashara amesema kwa sasa bendi yake haiwezi kupokea mwimbaji au mnenguaji bila kuwa na barua ya mwajiri wa zamani wa mwanamuziki hiyo alipotoka.
Bendi hiyo inataraji kununua basi kubwa na fuzo kwaajili ya kubeba vyombo na wanamuziki. Pia inataraji kufanya ziara ya mikoa ya Lindi tar 29-01-2009 na Mtwara tar 30-01-2009 kisha kuwaburuduisha wabunge na wana Idodomya wote 06-02-2009.
0 comments:
Post a Comment